Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Laptev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Laptev

Bahari ya Laptev ni bahari ya pembeni ya Bahari ya Aktiki kaskazini kwa Urusi. Iko kati ya pwani ya kaskazini ya Siberia, rasi ya Taimyr, Severnaya Zemlya na Visiwa vya Siberia Mpya. Eneo ni la км² 672.000.

Iko katikati ya Bahari ya Kara kwenye magharibi na Bahari ya Mashariki ya Siberia.

Mto Lena ni mto mkubwa unaoishia hapa katika delta pana.

Tabianchi ni baridi sana. Kutokana na latitudo karibu na ncha ya kaskazini usiku wa majirabaridi na mchana wa majirajoto hudumu miezi kadhaa.

Halijoto ya hewa iko chini ya sentigredi 0 kwa miezi 11 kila mwaka. Sehemu kubwa ya mwaka bahari imefunikwa na ngao ya barafu inayoweza kukua hadi unene wa mita 20-25.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.