Autism

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tabia za kawaida, hupanga vitu juu.

Tawahudi au Autism ni tatizo la kiroho na kihisia linalotokea kwa watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na watu wengine. Watu wenye matatizo ya autism hawaonekani kama watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuwaangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana mambo mengine na watu wengine. Pia, hawapo vizuri katika kimawasiliano. Muda mwingine wanakuwa hawawezi kuongea, au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wao wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine ambaye hana matatizo ya autism asifikirie kama kina umuhimu. Mtu mwenye tatizo hili anaelekea mara nyingi kurudiarudia matendo kadhaa, na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoelewka kama tatizo na wengine.

Dalili za autism[hariri | hariri chanzo]

Kukaa peke yake[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa kawaida asiye na autism huwaangalia watu wakizungumza, hutazama wengine usoni, hutabasamu, na huwa na shauku na watu wengine. Watoto wenye autism, wanaweza kupenda vituvitu zaidi kuliko sura au watu wengine. Wanaweza wakatazama usoni kwa sekunde tu, halafu mara moja akageuka. Wanaweza wasitabasamu, au wanaweza wakatabasamu kwa kitu kile alichokipenda.

Watoto wenye matatizo ya autism huwa na kawaida ya kukaa wenyewe tu, bila kuwepo kwa wengine. Wanaweza wasiwe na shauku ya kutaka urafiki na mtu yeyote. Pia, wanaweza wasiwe wanafanya kawaida kama kukumbatiana na alama nyingine za upendo kwa wazazi wao. Hii haimanishi kama hawa wapendi wazazi wao, ni kwamba hawajui namna ya kusema hivyo vitu.

Wanaweza wasione hisia za watu wengine; kwa mfano, wanaweza wasione tofauti kubwa sana kati ya labda mzazi ana furaha ma ana uzuni. Wanaweza wakacheka na kulia kwa mara zisizoeleweka.

Kutozungumza[hariri | hariri chanzo]

Mtoto mweye autism anaweza asithubutu kuongea, maana, au kujaribu kuelewa maongezi kati ya mwenzie mwenye umri sawa. Kuna baadhi yao huwa hawaongei kabisa. Wengi wao hawawezi kuongea vizuri na watu wengine.

Kufanya vitu tena na tena zaidi[hariri | hariri chanzo]

Kuna baadhi ya maautistic hutumia muda mwingi kufanya vitu vimoja kwa mara nyingi na nyingi zaidi, au kuwa na shauku na vitu ambavyo si vya kawaida; kuna baadhi yao wanaweza kutumia muda mwingi kwa kujizungushia mkono wake, kutembea na visanamu vyao, au kuvipnga vitu kwa mpangilio mmoja. Watu wenye matatizo ya autism wanaweza wakatumia muda mkubwa kwa kupanga visanamu vyake kwa mstari mmoja au vyumbavyumba na wanaweza kusikia jazba pindi mtu akavivuruga pale katika eneo lake.

Baadhi yao hawataki badiliko lolote lile, na wanaweza wakafanya mambo yaleyale kila siku bila kubadilisha—kama vile kuto kula, wanapokula, wanavaa, wanapiga mswaki, au pale wanapokwenda shule—huwa na uzuni kama kuna badiliko lolote katika vitu hivyo. Pia, wanaweza wakawa na shauku na vitu vya ajabu na kutumia muda wao mwingi kujifunza vitu hivyo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Autism lilipewa jina kwa mara ya kwanza mnamo 1943. Leo Kanner alifanya utafiti huu kwa watoto wapatao 11 na akagundua vitu ambavyo si vya kawaida kuhusu wao. Aliita early infantile autism. Muda huohuo, daktari mwingine, Hans Asperger, akafanya utafiti mwingine karibuni kitu sawa. Alichogunda sasa kinaitwa Asperger syndrome, wakati alichogundua Leo Kanner kinaitwa autistic disorder, childhood autism, infantile autism, au tu autism.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: