Martyrologium Romanum
Martyrologium Romanum (kwa Kilatini: Kitabu cha Wafiadini cha Roma) ni kitabu rasmi cha liturujia ya Roma kwa kufanya siku kwa siku ukumbusho wa watakatifu wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki. Ni msingi wa kalenda ya watakatifu katika mwaka wa liturujia.
Kinatunza orodha rasmi lakini isiyodai kuwa kamili, hivi kwamba majimbo, nchi na mashirika vinaweza kuwa na nyongeza maalumu za kwao.
Toka zamani jina Martyrologium lilitumika kwa orodha za watakatifu na wenye heri waliopangwa kadiri ya tarehe ya sikukuu zao. Polepole vitabu vya mahali tofauti viliongezewa majina kutoka vitabu vingine na hatimaye mikusanyo ilifikia kiwango cha kimataifa.
Katika Kanisa la Kiorthodoksi, kitabu cha namna hiyo kinaitwa Synaxarion, na toleo refu zaidi Menologion.
Toleo rasmi la Kanisa la Roma liliidhinishwa mara ya kwanza na Papa Gregori XIII mwaka 1584. Limetolewa upya mwaka 2001 halafu 2004[1] kwa kuzingatia zaidi ushahidi wa historia kama ulivyoagiza Mtaguso wa pili wa Vatikano [2]. Toleo hilo linaorodhesha watu 7,000 hivi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
- ↑ Sacrosanctum Concilium, 92c
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Martirologio Romano toleo rasmi kwa lugha ya Kiitalia
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Martyrologium Romanum kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |