Mkusanyo wa Sheria za Kanisa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mkusanyo wa sheria za Kanisa)
Mkusanyo wa Sheria za Kanisa (la Kilatini) ni kitabu ambamo zimekusanywa kwa mpango sheria kuu za Kanisa Katoliki zinazohusu waamini wake wa mapokeo ya Kilatini. Kwa lugha asili ya Kilatini unaitwa Codex Iuris Canonici(kifupi: CIC).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mkusanyo unaotumika kuanzia Majilio ya mwaka 1983 umeshika nafasi wa ule wa kwanza, uliotolewa mwaka 1917 kwa juhudi za Papa Pius X na halafu Papa Benedikto XV).
Urekebisho wake uliagizwa na Papa Yohane XXIII tarehe 25 Januari 1959 ukashughulikiwa na Papa Paulo VI na Papa Yohane Paulo II kufuatana na Mtaguso wa pili wa Vatikano.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kanuni zote za Mkusanyo huo katika Tovuti ya Vatikani
- Kamati ya Papa kwa Ufafanuzi Rasmi wa Sheria za Kanisa
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkusanyo wa Sheria za Kanisa kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |