Mkoa wa Rukwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mkoa wa Rukwa
Mahali paMkoa wa Rukwa
Mahali paMkoa wa Rukwa
Mahali pa Mkoa wa Rukwa katika Tanzania
Majiranukta: 7°0′S 31°30′E / 7.000°S 31.500°E / -7.000; 31.500
Nchi Tanzania
Wilaya 4
Mji mkuu Sumbawanga
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Daniel Ole Njoolay
Eneo
 - Jumla 75,240 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - Wakazi kwa ujumla 1,141,743
Tovuti:  http://www.rukwa.go.tz/
Mkoa wa Rukwa

Rukwa ni moja kati ya mikoa 26 za Tanzania. Inapakana na mikoa ya Kigoma na Tabora upande wa Kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa la Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia. Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.

Eneo la mkoa ni takriban 70,000 km². Kusini mwa mkoa liko ziwa la Rukwa ambalo ni kati maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki.

Wilayaa

Wilaya nne ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Sumbawanga Mjini (147,483), Sumbawanga Vijijini (373,080), Mpanda (412,683) na Nkansi (208,497).

Wakazi

Kuna wakazi 1,141,743 (sensa 2002).

Kabila kuwba zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Kati ya makabila mengine ni Wabende, Wapimbwe, Warungwa na Wakonongo katika wilaya ya Mpanda; Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamassai.

Viungo vya nje

Matokeo ya sensa 2002: en [1]

Makabila na lugha za Tanzania: en [2]


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Rukwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.