Jimbo Katoliki la Ifakara
Mandhari
Jimbo katoliki la Ifakara (kwa Kilatini "Dioecesis Ifakarensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Makao makuu yako mjini Ifakara.
Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Dar-es-Salaam.
Askofu wake ni Salutaris Melchior Libena.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 14 Januari 2012: Kuanzishwa kama Dayosisi ya Ifakara kutokana na maeneo ya jimbo la Mahenge
Maaskofu
[hariri | hariri chanzo]- Salutaris Melchior Libena (tangu 2012.01.14)
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo ni la kilometa mraba 14,245, ambapo kati ya wakazi 322,779 (2012) Wakatoliki ni 287,000 (88.9%) katika parokia 18.
Wanahudumiwa na mapadri 62 (42 wanajimbo na 20 watawa (kwa wastani kila mmojawao anahudumia waumini 4.629). Pia kuna mabruda 3 na masista 198.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Ifakara kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |