Ifakara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ifakara kwa macho ya ndege

Ifakara ni makao makuu na ni kata ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania na kitovu cha eneo lenye mashamba makubwa ya miwa na yenye Postikodi namba 67501 katka Misimbo mipya ya posta. Kuna kituo muhimu cha TAZARA.

Mji uko katika bonde la mto Kilombero takriban kilomita 420 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam.

Ifakara ni mji mkubwa kuliko yote ya wilaya ya Kilombero, wenye makabila makuu mawili maarufu kama Wapogoro na Wandamba, wenye mfanano wa kuelewana katika baadhi ya matamshi ya lugha zao.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,956 [1] walioishi humo.

Taasisi muhimu mjini ni Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute) inayofanya uchunguzi wa kisayansi wa magonjwa kama malaria na ukimwi. Kanisa Katoliki linaendesha Hospitali ya St Francis inayotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya pamoja na chuo cha wauguzi.

Tangu tarehe 14 Januari 2012 mji ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Ifakara.

Jina

Jina Ifakara lilitokana na neno ufwakara lenye maana amekwishakufa. Neno hilo tena lilitokana na nyoka mkubwa ambaye alikuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo: watu mbalimbali waliuawa na mifugo pia kuuawa.

Jitihada nyingi zilifanyika kumuangamiza nyoka huyo na mwishowe walifanikiwa kumuua, ndipo neno ufwakara lilipovuma kwamba amekwishakufa. Wageni wengi kutoka sehemu tofautitofauti walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kutamka Ifakara, mpaka leo Ifakara ndilo jina kuu la mji huo ndani ya wilaya ya Kilombero.

Picha za Ifakara

Marejeo

  1. Sensa ya 2012, Morogoro - Kilombero DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-03.

Viungo vya nje

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kilombero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Ching'anda | Chisano | Chita | Idete | Ifakara | Igima | Kalengakelo | Kamwene | Katindiuka | Kibaoni | Kiberege | Kidatu | Kisawasawa | Lipangalala | Lumemo | Mang’ula 'B' | Mang'ula | Masagati | Mbasa | Mbingu | Mchombe | Michenga | Mkula | Mlabani | Mlimba | Mngeta | Mofu | Msolwa Station | Mwaya | Namwawala | Sanje | Signal | Utengule (Kilombero) | Viwanja Sitini


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ifakara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.