Kidatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidatu

Kidatu ni kata ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67508. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 32,589 [1] walioishi humo.

Iko kando ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa iliyopo upande wa kaskazini karibu na mto Ruaha Mkuu, pale inapotoka milimani na kuingia katika tambarare ya Kilombero. Milima hiyo inasaidia kuongeza uchumi wa taifa kwa sekta ya utalii hapa nchini.

Inapakana na hifadhi ya wanyama ya Selous upande wa kusini.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi ya wakazi hutegemea kilimo. Ajira inapatikana kwenye mashamba ya sukari ya Illovo.[2]

Kuna pia kiwanda cha sukari cha Illovo.[3]

Lambo la Kidatu la TANESCO ambalo lipo karibu ni asili ya sehemu kubwa ya umeme kwa taifa.

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Kidatu ni mahali ambako reli za TAZARA na Reli ya Kati huunganishwa kwa njia ya reli kutoka Kilosa. Kuna mitambo ya kubadilisha magari ya reli kutoka upana mkubwa wa reli ya TAZARA na upana mdogo wa Reli ya Kati.

Pia kuna barabara inayounganisha kata hiyo na wilaya ya Kilosa na kata nyingine za wilaya ya Kilombero[4][5].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kilombero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Ching'anda | Chisano | Chita | Idete | Ifakara | Igima | Kalengakelo | Kamwene | Katindiuka | Kibaoni | Kiberege | Kidatu | Kisawasawa | Lipangalala | Lumemo | Mang’ula 'B' | Mang'ula | Masagati | Mbasa | Mbingu | Mchombe | Michenga | Mkula | Mlabani | Mlimba | Mngeta | Mofu | Msolwa Station | Mwaya | Namwawala | Sanje | Signal | Utengule (Kilombero) | Viwanja Sitini


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kidatu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.