Nenda kwa yaliyomo

Waamhara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amhara)
Waamhara
Idadi ya Watu
25,120,000+
Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana
 EthiopiaEthiopia:
19,870,651[1]

 MarekaniUnited States:
83,000[2]
 SudanSudan:
79,000[2]
 SomaliaSomalia:
57,000[2]
 EritreaEritrea:
31,000[2]
 KanadaCanada:
16,000[2]
 YemenYemen:
9,200[2]
 UjerumaniUjerumani:
5,800[2]
Bendera ya Jibuti DjiboutiDjibouti:
4,200[2]
Bendera ya Misri EgyptEgypt:
2,900[2]
 IsraelIsrael:
2,100[2]

Mfalme Sahla Sellase
Mfalme Menelik II
Malkia Zauditu
Mfalme Haile Selassie
Shlomo Molla
Tewodros II

Waamhara (kwa Kiamhara: አማራ, kwa Ge'ez: አምሐራ) ni kabila la watu waishio katikati ya nchi ya Ethiopia. Ndilo la asili la nyanda za juu za kati nchini.

Idadi ya watu wanaozungumza lugha ya Kiamhara, wanakadiriwa kufikia milioni 19.8, kiasi cha asilimia 26 ya wakazi wote wa nchi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2007. Huongea lugha ambayo imekuwa lugha ya wafanyakazi na taasisi za serikali na za jamii, pia ya siasa na uchumi nchini humo.

Kutokea kwa jina la ""Amhara"" bado ni swala linalojadiliwa. Kwa mujibu wa baadhi ya watu wanadai kuwa, neno "amari" linamaanisha "kuridhisha" ""kukubali" "uzuri" au "asante". Baadhi ya wanahistoria wa nchini Ethipia kwa mfano Gatachew Makonnen Hasen wanadai kuwa jina hilo lina lina uhusiano la jina la Himyarites.[3]. Huku wengine wakidai kuwa, jina hilo likiwa na uhusiano na kabila la Ge'ez likimaanisha "watu huru", yaani ዓም "ʿam" ikimaanisha "watu" ሓራ ""h.ara"" ikimaanisha "huru" au "mwanajeshi". Huku kwa upande mwingine waandishi kama Donald Levine akipinga mawazo haya juu ya historia ya jina hili. .[4]

Lakini kwa ujumla, jina hili linatokana na makabila ya eneo hilo ya zamani, yaliyokuwa yakiishi katika jimbo la Amhara lililopo kati mwa Ethiopia, na sasa likiwa tayari limeshakuwa Mkoa wa Amhara. Hii ikiwa ni kutokea mwaka 1995.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kumekuwa na watu wa kabila la Agazya, walijenga Ufalme wa Aksum kiasi cha milenia mbili zilizopita, na hii ikapanua ile inayojulikana sasa kama Eritrea na Ethiopia ya kaskazini, na wakati mwingine visehemu katika nchi za Yemen na Sudan.

Watu wa kabila la Amhara walirithi dini na mfumo wa uongozi wa kifalme kutoka katika Axum.

Jimbo ambalo sasa linajulikana kama "Amhara" katika kipindi cha ukabaila, eneo la watu wa Amhara lilijumuisha majimbo kadhaa kama vile, Begemder, Gojjam, Qwara na Lasta. Maeneo mengine ya nchini Ethiopia yenye idadi kubwa ya watu wa kabila la Amhara ni pamoja na Shewa na Gojjam.

Wanahistoria kwa ujumla wana imani ya kuwa, watu wa kabila la Amhara, kuwa ndilo linaloongoza kwa kutoa viongozi wengi katika nafasi mbalimbali, kuanzia Haile Selassie, mfalme wa mwisho wa Ethiopia. Lakini wachangiaji wengine kama vile Marcos Lemma wanaona kuwa si hivyo, kwani hata makabila mengine yameonekana kuchangia katika siasa za nchini humo.

Dini ya Waamhara kwa karne nyingi ni Ukristo, huku makanisa mengi ya zamaji ya nchini Ethiopia yakiwa muhimu katika utamaduni wa nchi hiyo.

Dini hiyo imekuwapo katika eneo hili kwa karne kadhaa sasa. huku Wakristo wa imani sahihi wakiwa kama sehemu muhimu katika utamaduni wa nchini mwao.

Nchini Ethiopia kwa jumla Wakristo ni 62.8% za wakazi wote, na kati yao Waorthodoksi wa mashariki ni 43.5%. Lakini katika Amhara asilimia kubwa kabisa ni Wakristo wa aina hiyo.

Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia linaendeleza ushirikiano na Kanisa la Misri.

Kufuatana na mapokeo ya huko, Epifania na Pasaka ni sikukuu muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile kufunga kula na kucheza. Pia kuna siku kadhaa katika mwaka ambapo ni mboga za majani pekee na samaki ndio huruhisiwa kuliwa.

Ndoa huweza kuanzishwa au kupangwa wakati mwanamume ana umri wa miaka kumi na..., au ishirini na... Kiutamaduni, wasichana wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika karne ya 20, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na serikali. Ndoa za kiserikali ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la talaka halipo na haliwezekani. Kila familia hufanya sherehe ya ndoa baada ya harusi.

Tangu kuzaliwa, padri hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki mtoto, na pia kutahiri mtoto kama ni wa kiume. Mama wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya ubatizo.

Sanaa ya nchini Ethiopia kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini. Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye macho makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na Biblia.

Kiasi cha asilimia 90 ya watu wa kabila la Amhara wanaishi katika maeneo ya vijijini, na hivyo sehemu kubwa ya maisha yao hutegemea kilimo, ambao wengi wao hufanya shughuli za kilimo katika ukanda wa juu wa Ethiopia.

Tangu mwaka 1974, baada ya mapinduzi ya Ethiopia na kuondolewa kwa utawala wa wakuu wa ardhi, watu wa kabila la Amhara wamekuwa makini sana katika umilikaji wa ardhi. Baada ya mwaka 1974, watawala wa ardhi waliondolewa na nafasi zao kuchuliwa na viongozi wa serikali ambao pia walifanya kazi zilezile.

Mazao kama vile shayiri mahindi, mpunga, ulezi na maharagwe hulimwa kwa wingi na watu wa jamii ya Amhara, pia hulimwa mboga za majani mbalimbali. Ulimwaji wa aina moja ya mazao kwa mwaka mzima ni jambo la kawaida katika nyanda za juu wakati katika nyanda za chini, huweza kulima aina hata mbili za mazao kwa mwaka.

Pia jamii hufuga mifugo mbalimbali kama vile ng'ombe, kondoo, na mbuzi.

  1. "Census 2007" Ilihifadhiwa 4 Juni 2012 kwenye Wayback Machine., first draft, Table 5.
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 "Joshua Project - Amhara, Ethiopian Ethnic People in all Countries". U.S. Center for World Mission. Iliwekwa mnamo 2008-11-05.
  3. Getachew Mekonnen Hasen, Wollo, Yager Dibab (Addis Ababa: Nigd Matemiya Bet, 1992), p. 11.
  4. Herausgegeben von Uhlig, Siegbert, Encyclopaedia Aethiopica: A-C. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag, 2003. pp. 230.
  • Wolf Leslau and Thomas L. Kane (collected and edited), Amharic Cultural Reader. Wiesbaden: Harrassowitz 2001. ISBN 3-447-04496-9.
  • Donald N. Levine, Wax & Gold: Tradition and Innovation in Ethiopian Culture (Chicago: University Press, 1972) ISBN 0-226-45763-X

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waamhara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.