Barack Obama
Barack Obama | |
6 Desemba 2012 | |
Aliingia ofisini Januari 20, 2009 | |
Makamu wa Rais | Joe Biden |
mtangulizi | George W. Bush |
aliyemfuata | Donald Trump |
Muda wa Utawala Januari 3, 2005 – Novemba 16, 2008 | |
mtangulizi | Peter Fitzgerald |
aliyemfuata | Roland Burris |
Muda wa Utawala January 8, 1997 – November 4, 2004 | |
mtangulizi | Alice Palmer |
aliyemfuata | Kwame Raoul |
tarehe ya kuzaliwa | Agosti 4 1961 Honolulu, Hawaii, U.S. |
utaifa | American |
chama | Democratic |
ndoa | Michelle LaVaughn Robinson (m. 1992–present) |
mahusiano | Stanley Armour Dunham (grandfather) Madelyn Lee Payne (grandmother) Maya Kassandra Soetoro-Ng (half-sister) |
watoto | Malia Ann Obama (b. 1998) Natasha Obama (b. 2001) |
makazi | Chicago, Illinois |
mhitimu wa | Occidental College Chuo Kikuu cha Columbia (B.A.) Harvard Law School (J.D.) |
Fani yake | Lawyer Professor of constitutional law Community organizer Author |
dini | Ukristo |
Awards | Tuzo ya Nobel ya Amani |
signature | |
tovuti | barackobama.com |
Barack Hussein Obama II (amezaliwa 4 Agosti 1961) alikuwa rais wa 44 wa Marekani. Ni Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kushika wadhifa huo, na pia mtu wa kwanza mwenye kuzaliwa Hawaii kuwa rais wa Marekani.
Obama awali alihudumu kama Seneta mdogo kutoka jimbo la Illinois, tangu Januari 2005 hadi alipojiuzulu baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008, mwezi wa Novemba.
Obama alifuzu mwanzo kutoka katika chuo kikuu cha Columbia University, kisha akafuzu katika masomo ya sheria kutoka katika kitivo cha masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Harvard, ambako alikuwa rais wa jarida la Harvard Law Review.
Alihudumu baadaye kama mwanaharakati wa mambo ya kijamii, kabla ya kuhitimu katika masomo ya kisheria.
Hatimaye, alifanya kazi kama wakili wa haki za umma mjini Chicago, kisha akafunza sheria ya kikatiba katika Chuo Kikuu cha Chicago kuanzia 1992 hadi 2004.
Obama alihudumu mihula mitatu katika Bunge la jimbo la Illinos (Illinois Senate) tangu 1997 hadi 2004. Baada ya kushindwa katika jitihada zake za kuchaguliwa katika Bunge Dogo la Marekani mwaka 2000, Obama alisimama kuchaguliwa katika Bunge La Maseneta La Marekani mwaka 2004. Alishinda uchaguzi hapo Novemba 2004.
Alitangaza kusimama kuchaguliwa kama rais wa Marekani mwezi Februari, mwaka 2007. Baada ya kampeni kali katika uteuzi wa chama cha Democratic Party dhidi ya Hillary Clinton, aliteuliwa kama mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho. Katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2008, alimshinda John McCain, aliyekuwa ameteuliwa na chama cha Republican Party, akaapishwa kama rais tarehe 20 Januari 2009.
Tarehe 9 Oktoba 2009, Obama alituzwa kwa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Mwaka 2012 alishinda tena uchaguzi mkuu na kuendelea kuongoza hadi tarehe 20 Januari 2017, alipompisha Donald Trump.
Utoto na Ujana
Baba yake Obama alikuwa Mjaluo wa Kenya Barack Obama aliyeaga dunia 1982. Mzee Obama alitoka mkoa wa Nyanza nchini Kenya akaenda Marekani masomoni. Mama yake, Ann Dunham, alikuwa Mwamerika Mzungu kutoka jimbo la Kansas aliyeaga dunia 1995.
Wazazi walioana wakati ndoa kati ya watu weupe na weusi bado ilikuwa marufuku katika sehemu za kusini za Marekani. Wazazi waliachana baada ya miaka miwili na mtoto Barack alibaki na mama.
Baadaye mama yake aliolewa na mwanafunzi kutoka Indonesia akamfuata aliporudi kwake. Hivyo Barack aliishi Jakarta hadi 1971 aliporudi Marekani na kukaa na babu yake huko Hawaii hadi alipomaliza shule ya sekondari.
Barack ana dada mmoja kutoka ndoa ya pili ya mama yake na baba ya kambo kutoka Jakarta, Indonesia
Masomo na kazi
Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alisomea masuala ya siasa na sheria katika vyuo vya Occidental huko Los Angeles, Columbia huko New York na baadaye chuo kikuu cha Harvard. Mwaka 1991 alimaliza kwa shahada ya dokta.
Baada ya shahada ya kwanza Obama aliwahi kufanya kazi ya kijamii huko Chicago. Mwaka 1991 alirudi Chicago alipopata kazi katika ofisi ya wanasheria akafundisha pia kozi za sheria kwenye chuo kikuu cha Chicago.
Kuingia katika siasa
Mwaka 1996 alichaguliwa kama seneta wa bunge la Illinois akarudishwa 1998 na 2002. Mwaka 2004 alichaguliwa kuwa seneta wa bunge la kitaifa.
Mwezi wa Februari 2007 alitangaza ya kwamba atatafuta nafasi ya mgombea wa urais upande wa chama cha kidemokrasia. Katika kampeni ya kitaifa ndani ya chama chake alifaulu kumshinda mgombea mwenzake mama Hillary Clinton. Tarehe 28 Agosti 2008 aliteuliwa na mkutano wa chama cha kidemokrasia kuwa mgombea wa chama hicho kwa urais. Katika uchaguzi wa Novemba 2008 alimshinda mgombea wa chama cha kijamhuri seneta John McCain.
Familia
Obama alimwoa Michelle Robinson ambaye ni mwanasheria kama yeye mwenyewe. Wana mabinti wawili Malia Ann (*1998) na Natasha (*2001) anayeitwa Sasha. Familia ina nyumba yake huko Chicago.
Urais
Obama aliongoza kama rais tangu Januari 2009 hadi Januari 2017.
Tuzo ya Nobel ya Amani
Mwaka wa 2009 aliteuliwa kwa Tuzo ya Nobeli ya Amani "kwa jitihada zake za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano kati ya mataifa".[1]
Marejeo
Viungo vya nje
- What makes Obama run? - Chigaco Reader 1995 juu ya Obama kama mgombea wa senati ya Illinois Archived 2 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- Official website
- Official website
- Official website
- Official website
- White House biography
- Barack Obama katika Open Directory Project
- Collected news and commentary kwenye Tampa Bay Times
- Collected news and commentary Archived 23 Machi 2019 at the Wayback Machine. kwenye The Washington Post
- "Barack Obama is officially one of the most consequential presidents in American history" iliandikwa na Dylan Matthews mnamo Machi 24, 2017.
- Archived from the original mnamo Machi 24, 2017.
- Works by Barack Obama katika Project Gutenberg
- Barack Obama at the Internet Movie Database
}}