Bill Clinton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bill Clinton.

William Jefferson Clinton (amezaliwa tar. 19 Agosti 1946), anafahamika zaidi kama Bill Clinton, alikuwa rais wa 42 wa Marekani. Alianza kutumikia taifa la Marekani kuanzia mnamo mwaka wa 1993 hadi 2001. Alivyo chaguliwa kuwa rais, alikwa na umri wa mika 46. Mpinzani wake mkubwa alikuwa mzee George H. W. Bush na Bw. Bob Dole.

Clinton alikuwa rais wa kwanza kutoka kizazi cha Baby Boom na alikuwa rais wa tatu kijana kutumikia taifa la Marekani. Clinton anatokea chama cha Kidemokrasia. Wasaidizi wa Clinton wanasema ya kwamba jamaa amesaidia kuinua uchumi wa Marekani kunako miaka ya 1990. Wakati urais wake, kulikuwa na majigambo na mabishano ya hapa na pale na Wanarepublicans (chama).

Kabla ya kuwa rais, Clinton alikuwwa gavana wa Arkansas kuanzia mwaka 1979 hadi 1981, vilevile mwaka 1983 hadi 1993 .

Mnamo mwaka 1994, wakati wa mhura wa kwanza Clinton kuingia ofisini, Baraza kuu la Marekani, lilikuwa linamilikiwa na Wanarepublican. Hata hivyo, Clinton aliendelea kumshinda mmoja wa wagombea Urais kutoka Republican Bw. Bob Dole, katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 1996 .

Rais Clinton alishtakiwa na Senati ya Marekani mnamo mwezi Desemba 1998 kwa kashfa za kusema uwongo mbele ya mahakama kuhusu mahusiano ya kimapenzi na Bi. Monica Lewinsky.

Kashfa hii ilimshushia hadhi yake kidogo.

Hata hivyo alikuwa rais aliyekubaliwa na raia wengi hadi mwisho wa kipindi chake. Alipoacha ikulu bajeti ya dola ilikuwa mara ya kwanza na ziada ya pesa tangu miaka 40.

Rais Clinton na Pele wakicheza mpira

.

Bill, amemwoa Seneta Hillary Clinton na kwa sasa wanaishi mjini New York.

Tazamia pia [hariri]

Viungo vya Nje [hariri]