John F. Kennedy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
John F. Kennedy

John Fitzgerald Kennedy (29 Mei 191722 Novemba 1963) alikuwa Raisi wa Marekani. Alikuwa mtoto wa pili katika familia ya watoto 9. Baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu. Ukoo wa Kennedy una asili ya Kiirish. Vita Kuu ya Pili ilipoanza alijiunga na jeshi la wanamaji. 1943 alijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na ndege za kivita za Japani. Mwaka 1947 alianza kujiingiza katika siasa na 1960 alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 22 Novemba 1963. Atakumbukwa pia kwa kutetea haki za watu wote bila kujali rangi.

Alisema "Wamarekani wasiulize Marekani imewatendea nini bali wajiulize kwanza wao wenyewe wameitendea nini nchi yao".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Administradors.gif Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John F. Kennedy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.