Nenda kwa yaliyomo

Kanisa la Magharibi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wakristo wa Magharibi)
Mitume Petro na Paulo walivyochorwa na El Greco katika karne ya 16, Hermitage Museum, Russia. Ndio walioathiri zaidi Ukristo wa Magharibi.

Kanisa la Magharibi (au Ukristo wa Magharibi) linajumlisha Kanisa la Kiroma-Katoliki pamoja na madhehebu ya Kiprotestanti. Huitwa "la magharibi" kwa sababu asili yake ni upande wa magharibi wa Bahari ya Kati yakiwa na mwelekeo tofauti na ile ya Makanisa ya Mashariki iliyoenea hata nje ya Dola la Roma.

Katika Karne za kati, taratibu Kanisa la Roma liliunganisha magharibi yote chini yake, hata kwa kufuta mapokeo tofauti, kama ya Makanisa ya Kiselti katika visiwa vya Britania.

Hata baada ya Kanisa la Magharibi kupatwa na mafarakano mengi, hasa katika karne ya 16, bado kuna mambo mengi yanayofananisha Kanisa la Kilatini na madhehebu mengi ya Uprotestanti yaliyotokana yote nayo ama moja kwa moja ama kupitia madhehebu yaliyokwishajitenga.

Ndiyo aina ya Ukristo iliyoenea zaidi duniani (85% hivi) pamoja na ustaarabu wa magharibi ulioathiriwa nayo, kiasi kwamba katika sehemu nyingi Ukristo wa Mashariki haujulikani au walau haueleweki.

Matawi ya Ukristo yalivyotokea katika historia ya Kanisa. Upande wa juu ndio Kanisa la Magharibi, upande wa chini Makanisa ya Mashariki. Unene wa mistari haulingani na ukubwa wa madhehebu husika.


Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Magharibi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.