Jimbo Katoliki la Isiolo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Vikarieti ya Kitume ya Isiolo)
Jimbo Katoliki la Isiolo (kwa Kilatini Diocesis Isiolana) ni mojawapo kati ya majimbo 28 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.
Liko chini ya jimbo kuu la Nyeri.
Lilianzishwa kama Vikarieti ya Kitume (Vicariatus Apostolicus Isiolansus) tarehe 15 Desemba 1995 kwa kumega Jimbo Katoliki la Meru. Kama dayosisi lilianzishwa tarehe 15 Februari 2023.
Makao makuu yako mjini Isiolo. Askofu ni Peter Munguti Makau, I.M.C.
Eneo lake ni kilometa mraba 25,336, ambamo mwaka 2023 kati ya wakazi 177,730 Wakatoliki walikuwa 69,070 (38.9% ya wakazi wote), wakigawanyika katika parokia 14. Mapadri ni 26, wakiwemo wanajimbo 21 na wanashirika 5. Watawa wa kiume ni 6 na wa kike ni 78.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- (Kilatini) Hati Ad aptius
- (Kilatini) Hati Aedificavit sibi domum, AAS 115 (2023), pp. 269–270
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Catholic-hierarchy.org
- (Kiingereza) Tovuti ya Baraza la Maaskofu
| Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Isiolo kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |