Nenda kwa yaliyomo

Ruvu (Pwani)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ruvu (pwani))

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Ruvu (maana)

Ruvu (pwani)/Ruvu au Kingani
Ruvu (au Kingani) mnamo mwaka 1910 karibu na mdomo wake Bagamoyo
Chanzo Milima ya Uluguru, mitelemko ya mashariki
Mdomo Bahari Hindi, karibu na Bagamoyo
Nchi Tanzania
Urefu km 285
Tawimito upande wa kulia Mto Mgeta
Tawimito upande wa kushoto Mto Ngerengere
Eneo la beseni km² 17,700

Ruvu (zamani Kingani pia[1]) ni mto wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

Unapokea hasa maji ya upande wa mashariki wa milima ya Uluguru na kuyapeleka Bahari Hindi.

Ruvu hii haina uhusiano na mto Jipe Ruvu wa mkoa wa Kilimanjaro / Upare.

Beseni la mto

[hariri | hariri chanzo]

Beseni la mto lina eneo la takriban kilomita za mraba 17,700 [2]

Ndani yake kuna maeneo matatu ya utiririshaji yaani, Ruvu ya Juu, Ngerengere na Ruvu ya Chini. Ruvu ya Juu inapokea maji kutoka mtelemko wa mashariki wa Uluguru, Ngerengere kutoka mtelemko wa magharibi na Ruvu ya chini kutoka milima mingine.

Tabianchi ya beseni inabadilika kati ya mahali na mahali; milima ya juu hupokea mvua zaidi kuliko tambarare za chini. Mwezi unaoleta mvua nyingi ni Aprili.

Chanzo cha maji ya Dar es Salaam

[hariri | hariri chanzo]

Ruvu ya Pwani ni chanzo kikuu cha maji kwa jiji la Dar es Salaam. Hili ni tatizo kwa sababu kiasi cha maji yake huzidi kupungua kutokana na uharibifu wa misitu na mabadiliko ya tabia ya nchi.[3]

Tangu mwaka 1958 kiasi cha maji ya Ruvu kinapimwa kwenye daraja la barabara kuu A7 takriban kilomita 40 kabla ya mdomo wake. Kwa wastani zimepita hapa 61 kwa sekunde. Kiwango hiki kinabadilika sana kulingana na majira ya mvua na ya ukame.

Kiwango cha maji (mita za ujazo kwa sekunde) kinachopita kwenye daraja la Ruvuma karibu na Mlandizi kwa mwezi
(Ilikadiriwa kwa kutumia data za kipindi cha miaka 46 1958–2004)[4]

Serikali inapanga kujenga lambo na kuanzisha bwawa la Kidunda kwenye njia ya mto Ruvu takriban kilomita 70 upande wa kusini wa Chalinze. Bwawa hili linakusudiwa kudhibiti mwendo wa maji kwenye mto Ruvu na kuongeza maji kwa ajili ya vituo vya kuchukua maji ya Dar es Salaam (DAWASA) wakati wa ukame. [5][6]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Linganisha makala "Kingani" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani: "Kingani oder Ruwu (d. i. Fluß)" - yaani Kingani au Ruvu (maanake mto)"
  2. Developing Rating Curves in the Ruvu River Sub - basin, taarifa kwa mradi wa Tanzania Integrated Water, Sanitation and Hygiene (iWASH) Program
  3. Impact of climate variability on groundwater resources in Dar es Salaam, Tanzania Ilihifadhiwa 27 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine., by Praxeda Kalugendo, Groundwater & Climate in Africa conference in Kampala (Uganda), June 2008
  4. "HYDROLOGIC AND LAND USE/COVER CHANGE ANALYSIS FOR THE RUVU RIVER" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-09-13. Iliwekwa mnamo 2021-01-20.
  5. https://store.globaldata.com/report/dawasa-kidunda-water-supply-dam-tanzania/#product-1229893 DAWASA – Kidunda Water Supply Dam – Tanzania, globaldata.com 09.08.2018
  6. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/dar-kupata-chanzo-cha-maji-cha-uhakika--3756830 Dar kupata chanzo cha maji cha uhakika, Mwananchi 22 Machi 2022

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]