Mtumiaji:Kisare/sandbox
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania | |
---|---|
Kaulimbiu ya taifa: "Uhuru na Umoja" | |
Wimbo wa taifa: "Mungu ibariki Afrika" | |
Mahali pa Tanzania katika Afrika ya Mashariki | |
Ramani ya Tanzania | |
Mji mkuu | Dodoma |
Mji mkubwa nchini | Dar es Salaam |
Lugha rasmi | |
Lugha za taifa | Kiswahili |
Makabila | Kupita makabila 125 |
Dini (asilimia) | 63.1 Wakristo 34.1 Waislamu 1.5 Wakanamungu 1.2 dini asilia 0.1 wengine |
Serikali | Jamhuri |
• Rais • Makumu wa Rais • Waziri Mkuu • Spika • Jaji Mkuu | Samia Suluhu Hassan Philip Isdor Mpango Kassim Majaliwa Tulia Ackson Ibrahim Hamis Juma |
Uhuru kutoka Ufalme wa Muungano | 9 Desemba 1961 (Tanganyika) 10 Desemba 1963 (Zanzibar) |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 947 303[1] |
• Maji (asilimia) | 6.4[1] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 65 642 682[1] |
• Sensa ya 2022 | 61 741 120[2] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 84.033[3] |
• Kwa kila mtu | USD 1 326[3] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 227.725[3] |
• Kwa kila mtu | USD 3 595[3] |
Maendeleo (2021) | 0.549[4] - duni |
Sarafu | Shilingi ya Tanzania |
Majira ya saa | UTC+3 (Afrika Mashariki) |
Muundo wa tarehe | siku/mwezi/mwaka |
Upande wa magari | Kushoto |
Msimbo wa simu | +255 |
Msimbo wa ISO 3166 | TZ |
Jina la kikoa | .tz |
Tanzania (jina rasmi: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki, ndani ya ukanda wa maziwa makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi.
Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, upo kaskazini-mashariki mwa Tanzania.
Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,120[2], (nchi ya 24 duniani) kutoka 44,928,923 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2012, likiwa ongezeko la 3.2% kwa mwaka.
Msongamano ni wa watu 47.5 kwa km² (nchi ya 124 duniani).
Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 765,179), lakini Dar es Salaam ndilo jiji kubwa zaidi, lenye watu 5,383,728.
Miji mingine ni kama vile Mwanza (1,004,521), Arusha (616,631), Mbeya (541,603), Morogoro (471,409), Kahama (453,654), Tanga (393,429), Geita (361,671), Tabora (308,741) na Sumbawanga (303,986).[5]
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina "Tanzania" liliundwa kama mkusanyiko wa majina ya maeneo mawili yaliyoungana kuunda nchi: Tanganyika na Zanzibar.[6] Jina lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na serikali kutafuta jina fupi zaidi kuliko "Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar".
Mshindi alikuwa mwenyeji wa Dar es Salaam aliyeitwa Mohamed Iqbal Dar[7]. Alipendekeza kuunganisha herufi tatu za kwanza za TANganyika na ZANzibar akafikia "Tanzan". Hakuridhika bado, akaona nchi nyingi za Afrika zina majina yanayoishia na "ia" akaongeza herufi hizi. Mwenyewe alieleza baadaye chaguo lake kwamba aliamua kutumia "I" ya jina lake Iqbal na "A" ya jina la dhehebu lake analolifuata katika Uislamu la Ahmadiyya.[8]
Jina "Tanganyika" linatokana na maneno ya Kiswahili "tanga" na "nyika", yakiunda msemo "tanga nyikani". Wakati fulani inaelezwa kama marejeleo ya Ziwa Tanganyika. [9] Jina la Zanzibar linatokana na "zenji", jina la watu wa eneo hilo (inadaiwa lina maana ya "nyeusi"), na neno la Kiarabu "barr", ambalo linamaanisha pwani au ufukwe.[10]
Historia
[hariri | hariri chanzo](Kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)
Kabla ya uhuru nchi zote mbili, Tanganyika na Zanzibar, zilikuwa chini ya utawala wa Uingereza lakini hazikuwa makoloni ya kawaida.
Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza).
- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Tanzania". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2025). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2024. (Archived 2023 edition)
- ↑ 2.0 2.1 Ofisi ya Taifa ya Takwimu – Tanzania (Oktoba 2022). Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022: Matokeo ya Mwanzo (PDF) (Ripoti).
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Tanzania)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 14 Oktoba 2023.
- ↑ "Human Development Report 2023/24" (kwa Kiingereza). Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa. 13 Machi 2024. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 22 Machi 2023.
- ↑ Ofisi ya Taifa ya Takwimu – Tanzania (Desemba 2022). Administrative Units Population Distribution Report (PDF) (Ripoti) (kwa Kiingereza).
- ↑ "tanzania | Etymology, origin and meaning of the name tanzania by etymonline". www.etymonline.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-16.
- ↑ Gordon Kalulunga (2011-06-17). "KALULUNGA BLOG: Mfahamu aliyebuni Jina la Tanzania". KALULUNGA BLOG. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-28. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Mohammed Iqbal Dar: Mbunifu wa jina la Tanzania". Global Publishers. 2016-03-07. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Loading..." home.frognet.net. Iliwekwa mnamo 2022-06-16.
- ↑ "zanzibar | Etymology, origin and meaning of the name zanzibar by etymonline". www.etymonline.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-16.