Nenda kwa yaliyomo

Philip Mpango

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Philip Isdor Mpango)
Philip Mpango

Mpango mwaka 2024

Muda wa Utawala
31 Machi 2021  3 Novemba 2025
Rais Samia Suluhu
mtangulizi Samia Suluhu
aliyemfuata Emmanuel Nchimbi

Muda wa Utawala
Novemba 2015  30 Machi 2021
Rais John Magufuli
Samia Suluhu
aliyemfuata Mwigulu Nchemba

Muda wa Utawala
2015  2021
Appointed by John Magufuli
Constituency Aliyechaguliwa (2015–2020)
Buhigwe (2020–2021)

tarehe ya kuzaliwa 14 Julai 1957 (1957-07-14) (umri 68)
Mkoa wa Kigoma, Tanzania
utaifa Bendera ya Tanzania Tanzania
chama Chama Cha Mapinduzi
ndoa Mbonimpaye Mpango
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Philip Isdor Mpango (alizaliwa wilaya ya Buhigwe, Mkoa wa Kigoma, 14 Julai 1957) ni mwanasiasa, mwanachama wa chama cha siasa cha CCM na mtalaam wa uchumi kutoka nchini Tanzania. Alihudumu kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tangu mnamo 31 Machi 2021 baada ya kuteuliwa na rais wa sasa Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli[1] hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo aliamua asigombee tena.

Aliteuliwa na John Magufuli kuwa mbunge katika muhula wa 20152020, baadaye alichaguliwa kama mbunge wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma katika uchaguzi wa mwaka 2020. Mnamo 30 Machi 2021 aliteuliwa na kuthibitishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania[2].

Maisha ya awali na elimu

Mpango alisoma elimu ya msingi na sekondari na baadaye kidato cha tano na sita mkoa wa Kagera katika shule ya Secondari Ihungo.

Alipata shahada ya awali, shahada ya uzamili na kisha shahada ya uzamivu (PhD) katika uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Sehemu ya masomo yake ya PhD alisomea katika Chuo Kikuu cha Lund, nchini Uswidi, na hatimaye alikamilisha utafiti wake na kupata PhD katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo 1996.[3]

Kabla ya kuingia rasmi katika siasa, Mpango alihudumu katika nyadhifa mbalimbali kama mchumi mwandamizi katika Benki ya Dunia, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) pamoja na kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango katika Ofisi ya Rais.[4]

Waziri wa Fedha

Mpango aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania mnamo Desemba 2015 katika serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli. Alihudumu katika nafasi hiyo hadi Machi 2021. Wakati wa kipindi chake, alichukua hatua za kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani, kupunguza utegemezi wa misaada ya nje, na kuongoza bajeti zinazolenga miradi ya kimkakati ya maendeleo.[5]

Makamu wa Rais

Baada ya kifo cha Rais John Magufuli, Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Makamu wa Rais aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumteua Mpango kuwa Makamu wa Rais, uteuzi uliothibitishwa na Bunge mnamo 30 Machi 2021.[6] Aliapishwa rasmi siku iliyofuata, na kuwa Makamu wa Rais wa kwanza kutoka Tanzania bara tangu enzi za Ali Hassan Mwinyi.

Maisha binafsi

Dkt. Mpango ni mume na baba wa familia. Anafahamika kwa uchapakazi wake na msimamo wa uadilifu katika usimamizi wa fedha za umma. Ameendelea kushiriki mijadala ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika kupitia majukwaa mbalimbali ya kikanda.

Tanbihi

  1. "President Suluhu nominates Philip Mpango as Tanzania's new VP". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2021-03-30. Iliwekwa mnamo 2025-07-22.
  2. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/dk-philip-mpango-ni-nani--3342068
  3. "Hon. Dr. Philip Isdor Mpango, Nominated Member". Parliament of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-01. Iliwekwa mnamo 2025-07-21.
  4. "Philip Mpango Bio – Early Life, Career, Activities". UnitedRepublicofTanzania.com. Iliwekwa mnamo 2025-07-21.
  5. "Tanzania's re-elected leader keeps finance minister Mpango in new govt". Reuters. 13 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 2025-07-21.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "President Suluhu nominates Philip Mpango as Tanzania's new VP". Daily Nation. 30 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 2025-07-21.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Philip Mpango kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.