Ibrahim Hamis Juma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ibrahim Hamis Juma
binadamu
Jinsiamume Hariri
Tarehe ya Kuzaliwa15 Juni 1958 Hariri
Mahali alipozaliwaMusoma Hariri
AlisomaChuo Kikuu cha London, Lund University, Ghent University Hariri

Ibrahim Hamis Juma (amezaliwa 15 Juni 1958) ni wakili Mtanzania na Jaji Mkuu wa sasa wa Tanzania.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Amezaliwa katika wilaya ya Musoma Mjini katika wodi ya utawala ya Mukendo.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

-Shahada ya Sheria, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) -Mwalimu wa sheria, katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) -Mtaalam, Sheria ya Bahari, Chuo Kikuu cha Ghent, Ubelgiji -Mwalimu wa Sheria (sheria ya kimataifa ya haki za binadamu) Raoul Wallenberg Chuo Kikuu, Lund, Sweden -PhD,Sheria ya Bahari, University of Ghent, Ubelgiji [1] [2] [3] [4] [5] [6]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Aliwahi kufundisha chuo kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1980 mpaka 1990. Pia amefanya kazi kwa nidhamu na weledi mkubwa huku akiwa muumini mzuri wa dini ya Uislamu kipindi chote cha masomo yake pamoja na kazi.

Aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008 kabla ya kupandishwa cheo na kuitumikia Mahakama ya Rufaa mwaka 2012. Pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Tanzania (LRCT). [7] Aliteuliwa na Rais John Magufuli tarehe 10 Septemba 2017. Kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu, aliwahi kuwa Kaimu Jaji Mkuu na jaji katika Mahakama ya Rufaa. [8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibrahim Hamis Juma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.