Jimbo Kuu la Mombasa
Mandhari
Jimbo Kuu la Mombasa (kwa Kilatini Archidiocesis Mombasaën(sis)) ni mojawapo kati ya majimbo 28 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.
Ni makao makuu ya kanda ya Kanisa ya eneo la mashariki, ambayo inaundwa nalo na majimbo ya Malindi na Garissa.
Kwa sasa linaongozwa na askofu mkuu Martin Musonde Kivuva akiishi mjini Mombasa.
Eneo lake ni kilometa mraba 39,000, ambamo mwaka 2023 kati ya wakazi 2,854,855 Wakatoliki walikuwa 416,000 (14.6% ya wakazi wote), wakigawanyika katika parokia 61. Mapadri ni 142, wakiwemo wanajimbo 97 na wanashirika 45. Watawa wa kiume ni 64 na wa kike ni 615.