Jimbo Katoliki la Mpanda
Mandhari
Jimbo Katoliki la Mpanda (kwa Kilatini "Dioecesis Mpandensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Tabora.
Tarehe 21 Desemba 2018 Askofu wake Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga alipandishwa cheo kuwa askofu mkuu wa Mbeya.
Badala yake tarehe 13 Mei 2020 ameteuliwa askofu Eusebius Alfred Nzigilwa, ambaye kwa miaka 10 alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Ametawazwa tarehe 2 Agosti 2020.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Maaskofu wa Mpanda
- Eusebius Alfred Nzigilwa (2020 - )
- Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga (2014 - 2018 alipohamishwa)
- William Pascal Kikoti (2000 - 2012 alipofariki)
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo ni la kilometa mraba 46,346, ambapo kati ya wakazi 609,327 (2016) Wakatoliki ni 329,622 (54.1%).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Mpanda kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |