Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga (amezaliwa Bunda, Mkoa wa Mara, 3 Novemba 1966) ni askofu Mkatoliki nchini Tanzania.

Aliwekwa wakfu na kardinali Polycarp Pengo mwaka wa 2011 kama askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma.

Tangu tarehe 17 Februari 2014 hadi 21 Desemba 2018 alikuwa askofu wa Jimbo la Mpanda, halafu akateuliwa na Papa Fransisko kuwa askofu mkuu wa Mbeya na kusimikwa tarehe 28 Aprili 2019

Amekuwa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania mnamo Julai 2018).

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.