Baraza la maaskofu
Baraza la maaskofu (kwa Kiingereza Episcopal Conference) ni muundo wa Kanisa la Kilatini unaokutanisha maaskofu wa eneo fulani (kwa kawaida nchi huru fulani au nchi kadhaa, lakini pengine hata sehemu ya nchi kama hiyo ina maaskofu wengi sana).
Pengine ni wale tu wanaoongoza jimbo, pengine ni pamoja na waandamizi, wasaidizi au waliostaafu.
Pengine tena wanashiriki hata maaskofu wa eneo lile kutoka Makanisa Katoliki ya Mashariki.
Mabaraza ya namna hiyo zaidi ya 40 yalikuwepo kabla ya Mtaguso wa pili wa Vatikano ambao uliagiza yaanzishwe rasmi duniani kote (hati Christus Dominus, 38).
Kwa sasa yako 114, ambayo tena kwa kawaida yameunda mashirikisho ya kibara, kwa mfano "Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar" (kifupisho: SECAM).
Pamoja na ustawi huo, teolojia haijafafanua vya kutosha mamlaka ya mabaraza hayo kuhusiana na ile inayoeleweka zaidi ya kila askofu katika jimbo lake na ya Papa wa Roma katika Kanisa Katoliki lote.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya mabaraza yote by Giga-Catholic Information
- Hierakia ya Kanisa Katoliki by David M. Cheney
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Baraza la maaskofu kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |