Nenda kwa yaliyomo

Steve Biko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bantu Stephen Biko)
Steve Bantu Biko
Jina la kuzaliwa Steve Bantu Biko
Alizaliwa 18 Desemba 1946
Afrika Kusini
Alikufa 12 Septemba 1977, Pretoria
Nchi Afrika Kusini
Kazi yake Mwanaharkati wa kupiga vita ubaguzi wa rangi
Ndoa Ntsiki Mashalaba
Watoto Nkosinathi Biko, Lerato Biko,
Hlumelo Biko

Steve Bantu Biko (18 Desemba 194612 Septemba 1977) alikuwa mwanaharakati mwenye kupiga vita ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mnamo miaka ya 1960 na 1970.

Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi, baadaye akaanzisha vuguvugu la Black Consciouness Movement (Harakati za kujitambua kwa watu weusi). Vuguvugu hilo lilipata nguvu sana na kuenea haraka katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.

Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni na kuteswa na askari wa serikali ya kibaguzi. Biko alijulikana kama jabali la harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi. Wakati yupo hai, alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za kujaribu kuwatia nguvu watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake wa kusema kwamba "black is beautiful" akimaanisha kwamba "mtu mweusi ni mzuri." Alielezea maana ya msemo huu ni: "mtu, ni sawa kama ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.

Stephen Bantu Biko alizaliwa mjini King Williams Town, ndani ya jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini. Biko alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Natal Medical School.

Hapo awali Biko alikuwa akijishughulisha na masuala ya kutafuta "Umoja wa Umma wa Wanafunzi Afrika Kusini" (National Union of South African Students), baada ya kuweza kuwaadikisha watu weusi, wahindi, na watu weupe pia, kwamba wakiwa kama wanfunzi wanahitaji jumuiya itakayokuwa inawaangalia wanafunzi.

Kwa mpango huo aliweza kufanikisha kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wanafunzi nchini Afrika ya Kusini, kwa Kiingereza: South African Students' Organisation (Kifupi: SASO) mnamo miaka ya 1968, na Biko akachaguliwa kuwa kama rais wa kwanza wa juimuiya hiyo.

SASO pia ilikuwa na mahusiano ya kisiri na jumuiya ya Harakati za kujitambua kwa watu weusi (Black Consciousness Movement, Kifupi: BCM). Mke wa Biko bibie Ntsiki Mashalaba, alikuwa mchangiaji mzuri wa kundeleza jumuiya ya "Harakati za kujitambua kwa watu weusi".

Ntsiki na Biko kwa pamoja walizaa watoto wawili: mtoto wa kwanza alikuwa wa kike aliyejulikana kwa jina la Lerato, alizaliwa mnamo mwaka 1974, ambaye baadae alifariki akiwa na umri wa miezi miwili tu. Mtoto wa pili alikuwa wa kiume, allitwa Hlumelo, alizaliwa mnamo mwaka 1978, baada ya kifo cha Biko.

Mnamo mwaka 1972 Biko akawa rais wa kuzuga kuwa ndio rais anaeangalia kanuni za watu weusi (Kwa kiing: president of the Black People's Convention). Biko aliwekewa vikwazo wakati wa kipindi cha ubaguzi wa rangi umeshamiri mnamo Machi mwaka 1973. Lengo kuu la kumvisha kiremba cha ukoka bwana Biko, walimaansha ya kwamba Biko haruhusiwi kuzungumza na zaidi ya mtu mmjoa kwa wakati mmoja.

Biko aliwekewa hadi mipaka katika baadhi ya sehemu asikanyage kabisa yaani. Pia hakuruhusiwa kuzungumza mbele ya hadhara. Vile vile ilikatazwa kabisaa kuzungumzia dondoo za Biko alizokuwa akisema, ikiwemo tamko au maneno yoyote yale azumngumzayo bwana Biko.

Wakati Biko wamemuwekea vikwazo, harakati zake za kinchi zilizuiliwa katika jimbo la Eastern Cape, mahali alipozaliwa Biko. Baada ya Biko kurudi kule kwao alikozaliwa, akaanzisha tena jamii fulani iliyokuwa inaitwa "Jamii shinani" (kwa Kiing: Grassroots organizations) iliyoegemea hasa katika kutaka watu kujitegemea mwenyewe (self-reliance), jumuiya ilibeba taasi mbambali ikiwemo, community clinic, Zanempilo, the Zimele Trust Fund (ambaye baadae ilitoa msaada kwa familia yake wakati Biko alivyofungwa kisiasa), Njwaxa Leather-Works Project na Ginsberg Education Fund.

Kifo chake

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 18 Agosti ya mwaka 1977, Biko alitiwa nguvuni na polisi kwa thuhuma ya ugaidi kifungu namba 83 cha 1967 cha nchini Afrika Kusini. Steve Biko alipatwa na majelaha makubwa kichwani baada ya kukamatwa na mapolisi na kuanza kumpa kipigo kisichokuwa na kifani. Wakamfunga na minyororo katika kidirisha cha machuma kwa muda siku nzima.

Mnamo tarehe 11 Septemba ya mwaka 1977 mapolisi walimfunga Biko nyuma gari aina ya Land Rover, akiwa uchi, na kuanza kuendesha gari kwa umbali wa km 1,200. Alikufa mda mchache baada ya kujiri katika jela ya Pretoria, mnamo tarehe 12 Septemba ya mwaka 1977.

Polisi wakatangaza kwamba kifo chake kilisababishwa na njaa kali. Biko alikutwa na majeraha makubwa kichwani kwake, ambapo mengi yalionekana kama ushaidi mkali kuwa jamaa alifanyiwa kitendo cha kiukatili na hao waliomkamata. Kisha mwandishi wa habari na kiongozi wa kisiasa wa sasa, Bi. Helen Zille, alifuchua ukweli uliojificha juu ya kifo cha Biko.

Juu ya umaarufu wake, habari za kifo cha Biko zilienea haraka sana, macho ya watu walifunguka ulimwenguni kutambua ukatili wa ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendelea humo nchini Afrika ya Kusini. Mazishi yake yalihudhuliwa na mamia ya watu, wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wengine kutoka Marekani na Magharibi mwa Ulaya. Mwandishi wa habari mzungu wa Africa Kusini bwana Donald Woods, aliyekuwa rafiki wa karibu wa Biko, ambaye yeye ndio aliyepiga picha za majelaha ya kichwani kwa Biko, nae alihudhulia mazishi hayo.

Woods alilazimika kutoroka nchini Afrika Kusini na kuelekea Uingereza, ambapo alifanya kampeni mbalimbali zidi ya ubaguzi wa rangi na kuweka bayana zaidi habari za Biko kuhusu maisha yake mpaka kifo chake. Woods alindika habari mbalimbali, zikiwemo makala na vitabu pia vyenye kuhusu maisha na habari zote za Steve Bantu Biko.

Mwaka uliofuata tarehe 2 Februari 1978, jaji mkuu wa Eastern Cape alitoa tamko la kusema kwamba hatotoa hukumu kwa askari yoyote yule aliyehusika kwa kukamatwa na kutiwa kuizini kwa Biko. Wakati kesi inaendelea, ilitangazwa kuwa majelaha yote yaliyokuwa kichwani kwa Biko, ilikuwa ni kutaka kujaribu kujiua mwenyewe, na haikumaanisha kuwa Biko alipigwa.

Uongozi wa mahakama ulisema kwamba kesi haijapitishwa hukumu kwakuwa ilikosa msaada wa kiushahidi wenye kuonyesha kwamba Biko aliuawa. Mashtaka ya kuuwana yalikuwepo sema kilichokuwa kimefikiriwa ni hujma na sikingine, ila kwakuwa mauwaji yashatokea mnamo mwaka 1977, muda wa kotoa hukumu ukawa ushapita, hivyo hukumu ikawa imefeli.

Baada ya hujma na mazungushano ya huku na kule ikabidi iundwe "Tume ya ukweli na upatanishi" (Kwa Kiing:Truth and Reconciliation Commission), ambayo iliundwa kwa kufuata taratibu ndogo tu za kibaguzi, ilitaarifiwa mnamo 1997 kuwa moja kati ya maaskari watano wa kikosi cha usalama nchiini Afrika Kusini, alikubali kuwa yeye alichangia kuuawa kwa Biko, askari huyo ambaye alikuja kufa katika machafuko ya Soweto zidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.

Mnamo tarehe 7 Oktoba mwaka 2003 Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ilitangaza rasmi kwamba maaskari watano walioshtakiwa kwa kosa la mauwaji ya Biko, hawato hukumiwa kwasababu hakuna ushaidi wa kotosha, ukweli ni kwamba muda wa kutoa hukumu pia nayo ushapita, hivyo hamna hukumu yoyote ile zidi ya maaskari hao.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steve Biko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.