Maria Magdalena
Maria Magdalena, yaani wa Magdala (kwa Kigiriki: Μαρία ἡ Μαγδαληνή) ni mmoja kati ya wanafunzi maarufu zaidi wa Yesu wa Nazareti, hasa kutokana na sifa yake ya kuwa mtu wa kwanza kumuona amefufuka (Mk 16:9[1]; Yoh 20:16).
Kwa kuwa alitumwa naye kuwapasha habari hiyo Mitume, kuanzia Thoma wa Akwino anaitwa "Mtume wa Mitume"[2].
Habari zake kadiri ya Injili
[hariri | hariri chanzo]Ni kwamba, kadiri ya Injili, baada ya kushuhudia kifo cha Yesu na mazishi yake (Mk 15:40-16:1; Math 27:56-28:1; Yoh 19:25), upendo na juhudi vilimfanya mwanamke huyo awahi kwenye kaburi lake alfajiri ya siku ya Jumapili. Huko alitokewa na malaika na kuambiwa amefufuka.
Ndiye aliyewapasha habari hiyo mitume wa Yesu kabla hawajaenda kaburini na kulikuta halina maiti.
Baada ya Maria, hao pia walitokewa na Yesu mwenyewe, kuanzia mtume Petro.
Kabla hajaanza kumfuata, Maria alikuwa amepagawa na mapepo saba (Mk 16:9). Alipoponywa na Yesu, alijitolea kumhudumia na mali yake pamoja na wanawake wengine (Lk 8:2).
Habari yake kuu katika Yoh 20
[hariri | hariri chanzo]1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, "Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka."
3 Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini.
4 Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.
5 Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.
6 Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,
7 na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
8 Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyemtangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaaamini.
9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu).
10 Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani.
11 Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, akilia. Huku akiwa bado analia, aliinama na kuchungulia kaburini,
12 akawaona malaika wawili waliovaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja kichwani na wa pili miguuni.
13 Hao malaika wakamwuliza, "Mama, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Wamemwondoa Bwana wangu, na wala sijui walikomweka!"
14 Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu.
15 Yesu akamwuliza, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, "Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."
16 Yesu akamwambia, "Maria!" Naye Maria akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, "Raboni" (yaani "Mwalimu").
17 Yesu akamwambia, "Usinishike; sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."
18 Hivyo Maria Magdalene akaenda akawapa habari wale wanafunzi kuwa amemwona Bwana, na kwamba alikuwa amemwambia hivyo.
Heshima aliyopewa baada ya kufa
[hariri | hariri chanzo]Maria Magdalena anahesabiwa mtakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, akiadhimishwa tarehe 22 Julai[3]. Katika Kanisa la Kilatini Papa Fransisko ameipa hadhi ya sikukuu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionyesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo saba.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/23600
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Acocella, Joan. "The Saintly Sinner: The Two-Thousand-Year Obsession with Mary Magdalene." The New Yorker, 13 and 20 Februari 2006, p. 140–49. Prompted by controversy surrounding Dan Brown's The Da Vinci Code.
- Brock, Ann Graham. Mary Magdalene, The First Apostle: The Struggle for Authority. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press, 2003. ISBN 0-674-00966-5. Discusses issues of apostolic authority in the gospels and the Gospel of Peter the competition between Peter and Mary, especially in chapter 7, "The Replacement of Mary Magdalene: A Strategy for Eliminating the Competition."
- Burstein, Dan, and Arne J. De Keijzer. Secrets of Mary Magdalene. New York: CDS Books, 2006. ISBN 1-59315-205-1.
- Jansen, Katherine Ludwig. The Making of the Magdalen: Preaching and Popular Devotion in the Later Middle Ages. Princeton, N.J.: Princeton University Press, 2000. ISBN 0-691-05850-4.
- Kripal, Jeffrey John. (2007), The Serpent's Gift: Gnostic Reflections on the Study of Religion, Chicago: The University of Chicago Press, ISBN 0226453804 ISBN 0-226-45381-2.
- Pearson, Birger A. "Did Jesus Marry?." Bible Review, Spring 2005, pp 32–39 & 47. Discussion of complete texts.
- Picknett, Lynn, and Clive Prince. The Templar Revelation. New York: Simon & Schuster, 1997. ISBN 0-593-03870-3. Presents a hypothesis that Mary Magdalene was a priestess who was Jesus' partner in a sacred marriage.
- Shoemaker, Stephen J. "Rethinking the ‘Gnostic Mary’: Mary of Nazareth and Mary of Magdala in Early Christian Tradition." in Journal of Early Christian Studies, 9 (2001) pp 555–595.
- Thiering, Barbara. Jesus the Man: Decoding the Real Story of Jesus and Mary Magdalene. New York: Simon & Schulster (Atria Books), 2006. ISBN 1-4165-4138-1.
- Wellborn, Amy. De-coding Mary Magdalene: Truth, Legend, and Lies. Huntington, Indiana: Our Sunday Visitor, 2006. ISBN 1-59276-209-3. A straightforward accounting of what is well-known of Mary Magdalene.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "Saint Mary Magdalene." Encyclopædia Britannica Online.
- "St. Mary Magdalen", Butler's Lives of the Saints
- The Life of St. Mary Magdalene: Saint of the Christian Church Ilihifadhiwa 6 Mei 2015 kwenye Wayback Machine.
- St Mary Magdalene, Catholic Encyclopaedia 1911
- Convent of Saint Mary Magdalene Ilihifadhiwa 25 Julai 2017 kwenye Wayback Machine.
- St Mary Magdalen and the case for the ordination of women in the Catholic Church Ilihifadhiwa 2 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Legends of Mary Magdalene Ilihifadhiwa 9 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
- The Pesher Technique: The Marriage of Jesus by Barbara Thiering
- Miriam/Myriam M'Gadola: Mary Magdalene
- Articles and more than 40 Paintings Ilihifadhiwa 14 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- Early Christian Writings: Gospel of Mary
- Gospel of Mary Magdalene
- Showing inaccuracy of The Da Vinci Code in respect to Mary Magdalene
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maria Magdalena kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |