Lugha za Afrika
Mandhari
Lugha za Afrika ni zaidi ya 2000.
Baadhi ya lugha hizi zina wasemaji mamilioni kama vile Kiswahili, Kihausa, Kiigbo, au Kiyoruba. Lugha nyingine zina wasemaji wachache sana hata zinaelekea kupotea.
Vikundi vya lugha
Vikundi vikubwa vya lugha za Kiafrika ni hasa:
- Lugha za Kiafrika-Kiasia - lugha 350 zenye wasemaji milioni 350 katika Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi, hasa Kiarabu na Kiamhara
- Lugha za Kiniger-Kongo - lugha 1,400 zenye wasemaji milioni 370 katika Afrika ya Magharibi, mashariki na kusini Hizi ni pamoja na lugha za Kibantu kama Kiswahili.
- Lugha za Kisudani (Nilo-Sahara) - lugha 200 zenye wasemaji milioni 35 kati ya Sudani hadi Mali na Tanzania. Kati yake kuna Kijaluo na Kimaasai.
- Lugha za Khoisan - lugha 28 zenye wasemaji 355,000 katika Afrika ya Kusini na Tanzania. Wataalamu wanaelekea kuziona kuwa ndizo lugha zinazofanana zaidi na ile ya asili ya binadamu. Kati yake ipo lugha ya Wasandawe wa Tanzania.
Kuna pia maeneo penye wasemaji wa lugha zenye asili nje ya Afrika kama vile:
- lugha za Kiaustronesia katika Madagaska
- lugha za Kihindi-Kiulaya hasa katika Afrika ya Kusini halafu kama lugha rasmi kote Afrika kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kiafrikaans, Kihispania, Kitamil, Kigujarati, Kipunjabi na Kijerumani.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Afrika kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |