Lubumbashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Lubumbashi
Downtown Lubumbashi, Democratic Republic of the Congo - 20061130.jpg
Nickname: L'shi - Lubum
Lubumbashi is located in Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Lubumbashi
Lubumbashi
Mahali pa mji wa Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Viwianishi: 11°40′0″S 27°29′0″E / 11.66667°S 27.48333°E / -11.66667; 27.48333
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mikoa Katanga
Serikali
 - Governor Moise Katumbi
Eneo
 - Jiji 747 km²
Elevation 1,208 m (3,963 ft)
Idadi ya wakazi
 - 1,139,064

Lubumbashi (zamani ulijulikana Kifaransa: Élisabethville, au Kiholanzi Dutch: Elizabethstad) ni mji wa pili kwa ukubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani ilijulikana kama Zaire) ukifuata mji mkuu wa taifa wa Kinshasa na kitovu cha biashara cha sehemu ya kusini ya nchi. Mji huu ndio makao makuu ya Mkoa wa Haut-Katanga ambao una madini ya shaba na uko karibu na mpaka wa Zambia. Makadirio ya idadi ya watu inatofautiana sana lakini wastani ni karibu milioni 1.2 .

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Lubumbashi uko karibu mita 1,000 juu ya usawa wa bahari. Mto Kafue unatiririka kando ya mpaka wa Zambia na uaendelea kupitia sehemu za Zambia hadi Mto Zambezi.

Serikali[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia 2000-2006, Floribert Kaseba Makunko alikuwa meya wa Lubumbashi; baadaye alichaguliwa kwenye Bunge ya Taifa mwaka 2006.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wabelgigi walianzishwa mji wa Élisabethville (wakati mwingine Elizabethville , katika Kifaransa, au Elisabethstad katika Kiholanzi) mwaka 1910. Mji huu ulifanikiwa na maendeleo ya kanda hii kwenye sekta ya madini ya shaba.

Wachimbaji migodi katika Élisabethville waligoma Desemba 1941 katika kupinga serikali ya Wabelgigi iliyowalazimisha kufanya kazi ngumu , kwa sababu ya "jitihada za vita ".

Wabelgigi walanzisha Chuo Kikuu cha Élisabethville mnamo 1954-1955 (sasa Chuo Kikuu cha Lubumbashi). Katika uchaguzi wa manisipaa wa Desemba 1957, watu wa Élisabethville waliwapigia kura wengi wa wagombezi wa chama cha Nationalist Alliance de Bakongo, ambacho kilidai uhuru mara moja kutoka kwa Wabelgigi.

Élisabethville ulitumikia kama mji mkuu na kitovu cha biashara wa Jimbo la kujitenga la Katanga wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1960-1963. Moise Tshombe alitangaza uhuru wa Katangan Julai 1960. Viongozi wa Kongo walimtia nguvuni na kushtakiwa kwa uhaini Aprili 1961, hata hivyo,alikubali kufutilia washauri wake wa kigeni na vikosi vya kijeshi kubadilishana na uhuru wake. Tshombe alirejea Élisabethville lakini akakaidi mkataba na akaanza kupigana upya. Vikosi vya jeshi vya Umoja wa Mataifa vilipinga wanajeshi wa Katanga na kuchukua udhibiti wa mji mnamo Desemba 1961 chini ya mamlaka makuu. Roger Trinquier, anayejulikana kwa machapishwo yake kuhusiana na vita, alikuwa mshauri wa kijeshi Kifaransa wa Rais Tshombe mpaka shinikizo la kimataifa, ikiongozwa na Ubelgiji, zilisababishwa kuitwa tena na Ufaransa.

Mobutu Sese Seko hatimayea lipotwa mamlaka alibadilisha jina la Élisabethville hadi "Lubumbashi" na mwaka wa 1972 alibadilisha Katanga hadi "Shaba."

Kongo aliingia uangamizaji mwingine wa kivita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990. Waasi wa Muungano wa Democratic Forces kwa Ukombozi wa Kongo waliteka Lubumbashi mwezi Aprili 1997. Kiongozi wa waasi Laurent-Désiré Kabila alizungumza kutoka Lubumbashi kutangaza mwenyewe rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 17 Mei 1997 baada ya Mobutu Sese Seko kukimbia Kinshasa.

Wakati Laurent-Désiré Kabila aliamua kuteua bunge la mpito , mwaka 1999, uamuzi ulitolewa kufunya Bunge katika Lubumbashi, ili kuimarisha umoja tete wa nchi. Bunge liliwekwa katika jengo la Bunge la Wapinduzi wa Katanga, iliyokuwa na makao makuu yake katika jiji hili pia katika miaka ya 1960. Lubumbashi kwa hiyo ulikuwa mji wa mkuu wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia 1999 hadi 2003, wakati taasisi zote kuu za nchi zililetwa jijini Kinshasa.

Utamaduni na uchumi[hariri | hariri chanzo]

Lubumbashi unatumika kama kiungo muhimu cha kibiashara na viwanda vya kitaifa. Viwanda ni pamoja na viwanda vya nguo bidhaa za chakula na vinywaji, uchapishaji matofali, na uyeyushaji wa shaba. Kuna pia magazeti ya kila siku.

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Reli[hariri | hariri chanzo]

Lubumbashi ikko katika mstari wa reli baina ya Ilebo, Kindu, Sakania na Kolwezi, hata hivyo, kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu ya uwekezaji katika mfumo wa reli, reli wana sifa ya kutoaminika.

Katika miaka ya 1960, sehemu ya kutoka kwa Mutshatsha hadi Lubumbashi ilwekwa umeme wa hadi 25 KV AC.

Hewa[hariri | hariri chanzo]

Lubumbashi ni nyumbani kwa uwanja wa ndege wa kisasa wa Lubumbashi International Airport. Kwa hivyo,mji huu unatumika kama kituo cha usambazaji wa madini kama vile shaba, kobalti, zinki, stani na makaa ya mawe.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Benki ya kibiashara ya Kongo

Vivutio katika mji huu ni pamoja na bustani, mbuga ya wanyama Kiwanda cha Pombe na jumba la kumbukumbu la kanda la National Museum of Lubumbashi. Pia mji huu una Chuo Kikuu cha Lubumbashi, ambacho kina maktaba.

Kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:Anwani ya kijiografia: 11°40′S 27°28′E / 11.667°S 27.467°E / -11.667; 27.467

Flag-map of the Democratic Republic of the Congo.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lubumbashi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.