Nenda kwa yaliyomo

Kitukutuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kitukutuku
Distoleon tetragrammicus
Distoleon tetragrammicus
Lava wa D. tetragrammicus
Lava wa D. tetragrammicus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Neuroptera (Wadudu walio na mabawa wenye vena nyingi kama kimia)
Nusuoda: Myrmeleontiformia
Familia ya juu: Myrmeleontoidea
Familia: Myrmeleontidae (Vitukutuku)
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 4:

Vitukutuku au simba-sisimizi (kutoka Kiing. antlion) ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Myrmeleontidae katika oda Neuroptera (wadudu mabawa-vena) waliofanana kidogo na kereng'ende.

Jina linataja lava wa wadudu hao, lakini mara nyingi linatumika kwa wapevu pia. Lava wa spishi nyingi huchimba mashimo kwa umbo la mpare au marima ambamo wanakamata sisimizi wanaoanguka ndani, lakini spishi nyingine hazifanyi hivyo. Kuna takriban spishi 2000 zinazotokea mabara yote isipokuwa bara la Antakitiki.

Mpevu wa Myrmecaelurus trigammus
Lava wa Myrmeleon immaculatus

Wapevu wa vitukutuku wanaweza kuwa Neuroptera wadogo kiasi hadi wakubwa sana wenye upana wa mabawa wa kutoka sm 2 hadi zaidi ya 16. Jenasi ya Afrika Palpares ina baadhi ya spishi kubwa kabisa na P. voeltzkowi ya Madagaska ikiwa kubwa zaidi duniani yenye upana wa mabawa wa zaidi ya sm 16. Ya pili kwa ukubwa ni P. immensus yenye upana wa mabawa wa takriban sm 16[1]. Acanthaclisis occitanica ndiyo spishi kubwa kabisa ya Ulaya yenye upana wa mabawa wa sm 11 na spishi nyingi za Amerika ya Kaskazini hukaribia ukubwa huu[2].

Mpevu ana fumbatio ndefu na nyembamba na jozi mbili za mabawa marefu na membamba ambayo ni mangavu na kuwa na vena nyingi. Ingawa kwa kiasi fulani wanafanana na kereng'ende, hawana uhusiano. Wapevu wa vitukutuku wanatofautishwa kwa urahisi na kereng'ende kwa vipapasio vyao vionekanavyo wazi ambavyo vina kifundo nchani na urefu wa karibu kama kichwa na thoraksi pamoja[3]. Pia, ruwaza ya vena za mabawa hutofautiana na ikilinganishwa na kereng'ende wapevu wanaruka bila nguvu kabisa na kwa kawaida hupatikana wakipepea usiku wakitafuta mwenzi. Kwa kawaida wapevu hukiakia wakati wa usiku na hawaonekani mara nyingi wakati wa mchana[4].

Madume wa spishi nyingi wana muundo wa kipekee kwenye matako ya mabawa ya nyuma, kifundo chenye nywele ngumu kinachojulikana kama "pilula axillaris". Kwa kawaida fumbatio ya madume huwa ndefu kuliko majike na mara nyingi huwa na ndewe ya ziada. Ncha ya fumbatio ya majike huonyesha tofauti kubwa zaidi kuliko ile ya madume, kulingana labda na maeneo ya utagaji wa mayai, na kwa kawaida hubeba sekini za nywele ngumu kwa kuchimba na ugani kama kidole[5].

Kitukutuku ana mwili wenye nguvu. Fumbatio ni mnene sana na thoraksi inabeba jozi tatu za miguu ya kutembea. Prothoraksi huunda "shingo" nyembamba na nyumbufu kwa kichwa kikubwa, bapa na cha mraba kinachobeba jozi ya mataya makubwa sana kama miundu yenye michomozo kadhaa mikali iliyo na uwazi ndani. Mataya hayo huundwa kwa maxila na mandibuli. Kila mandibuli ina mfuo mrefu ambao juu yake maxila inabana vizuri, inayotengeneza mfereji uliozingirwa kwa kuingiza sumu ili kumzuia mwathiriwa[6][7] na vimeng'enya kwa kumeng'enya sehemu zake nyororo. Lava amevikwa nywele ngumu zinazoelekea mbele ambayo humsaidia kujitia nanga na kufanya mvutano mkubwa na kumwezesha kutiisha mbuawa mkubwa zaidi kuliko yeye[8]. Vitukutuku sio wa kawaida kati ya lava wa wadudu kwa kukosa mkundu. Takataka zote za kimetaboliki zinazozalishwa wakati wa hatua za lava huhifadhiwa. Baadhi hutumika kusokota hariri kwa kifukofuko cha bundo na mabaki hubatilika hatimaye mwishoni mwa hatua ya bundo na huitwa meconium[9].

Mzunguko wa maisha

[hariri | hariri chanzo]
Mzunguko wa maisha wa Distoleon tetragrammicus

Mbali na spishi zinazotengeneza marima, biolojia ya vitukutuku imechunguzwa kidogo. Mzunguko wa maisha huanza na utagaji wa mayai katika mahali panapofaa. Jike la kitukutuku hugonga tena na tena mahali pa kutaga kwa ncha ya fumbatio yake na kisha kuingiza neli ya kutagia yake ndani ya dutu ya chini na kutaga yai, ambalo hutoa lava baada ya mwezi mmoja hivi[10].

Kulingana na spishi na mahali inapoishi, lava hujificha chini ya majani, vifusi au vipande vya mbao au katika ufa au kuchimba shimo lenye umbo la mpare kwenye mchanga mtifu, ambapo hupitia hatua tatu[6]. Kama mbuai wa kuvizia, kukamata mbuawa ni hatari, kwa sababu chakula hufika bila kutabirika na, kwa zile spishi zinazotengeneza marima, kulitunza moja ni ghali. Kwa hivyo lava wana viwango vya chini vya kimetaboliki na wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila chakula[11]. Wanaweza kuchukua miaka kadhaa kukamilisha hatua zote. Wanakomaa haraka zaidi ikiwa chakula ni tele, lakini wanaweza kuishi kwa miezi mingi bila kujilisha[12][13]. Katika tabianchi za baridi huchimba mpaka kina kikubwa zaidi na kubaki bila shughuli wakati wa majira ya baridi[9].

Kifukofuko cha kitukutuku kwenye ukuta wa nyumba.

Wakati lava anapofikia ukubwa wake wa juu, hubadilika kuwa bundo na kufanya metamofosisi[13]. Hutengeneza kifukofuko cha mchanga au dutu nyingine ya eneo iliyoshikana pamoja na hariri laini iliyosokotwa kutoka kwa tezi nyembamba za kusokota kwenye ncha ya nyuma ya mwili. Kifukofuko kinaweza kuzikwa kwa kina cha sentimita kadhaa kwenye mchanga au kushikamana na vitu. Baada ya kukamilisha mabadiliko yake kuwa mdudu mpevu kwa muda wa mwezi mmoja hivi, hutoka kwenye kifukofuko na kuacha kutikulo ya bundo na kushughulika ili kufika kwenye uso. Baada ya dakika ishirini hivi, mabawa ya mpevu hufunguliwa kabisa na huruka kwenda kutafuta mwenzi. Mpevu ni mkubwa zaidi sana kuliko lava kwani vitukutuku huonyesha tofauti kubwa kabisa ya saizi kati ya lava na mpevu ya aina yoyote ya mdudu wa kiholometaboliki. Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba kiunzinje cha mpevu ni chembamba na dhaifu sana chenye msongamano wa chini sana[14]. Kwa kawaida mpevu huishi kwa takriban siku 25, lakini baadhi huishi kwa muda wa siku 45[13].

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]
Rima la kitukutuku katika mchanga

Vitukutuku hula arithropodi wadogo, hasa sisimizi, huku wapevu wa spishi fulani wakila mbelewele na mbochi na wengine ni mbuai wa arithropodi wadogo[15]. Katika baadhi ya spishi, kama vile Dendroleon pantherinus, lava, ingawa wanafanana na wale wa Myrmeleon kimofolojia, hawachimbi rima lakini hujificha ndani ya shimo katika mti na kukamata mbuawa anayepita[16]. Huko Japani, lava wa Dendroleon jezoensis huotea juu ya uso wa miamba kwa miaka kadhaa wanapongojea mbuawa. Wakati huu watafunikwa mara nyingi kwa kuvumwani na wamerekodiwa kuwa kwa misongamano ya hadi 344 kwa kila mita ya mraba[17].

Lava ni mbuai mkali. Ndani ya dakika chache baada ya kukamata mbuawa wake kwa mataya yake na kuingiza sumu na vimeng'enya, huanza kufyonza vizao vya mmeng'enyo[6][8]. Lava ni nyeti sana kwa mitetemo ya ardhi, sauti za marudio ya chini zinazotolewa na mdudu anayetambaa ardhini. Lava hupata chanzo cha mitetemo kwa tofauti za miuda ya kuwasili kwa mawimbi yaliyogunduliwa na vipokezi vya hisia, sekini za nywele kwenye pande za pingili mbili za nyuma za thoraksi[18].

Kitukutuku aliyevutwa kwenye rima.

Katika spishi zinazotengeneza marima lava wa ukubwa wa wastani huchimba shimo lenye kina cha sm 5 na upana wa sm 7.5 ukingoni. Tabia hii pia imeonwa katika Vermileonidae (Diptera), ambao lava wao huchimba shimo la aina sawa ili kujilisha kwa sisimizi. Baada ya kutopoa mahali palipochaguliwa kwa mfuo wa mviringo[19], lava huanza kutambaa kinyumenyume kwa kutumia fumbatio yake kama plau ili kusukuma mchanga juu. Kwa msaada wa mguu mmoja wa mbele anaweka mifululizo ya vilundo vya chembe zilizolegea juu ya kichwa chake, kisha kwa mshtuko mwepesi hutupa kila kilundo nje ya eneo la operesheni. Akifanya hivyo huendelea hatua kwa hatua kutoka kwa mzingo kuelekea kati[4]. Inaposogea polepole kuzunguka na kuzunguka, shimo polepole huingia ndani zaidi na zaidi hadi pembe ya mteremko ifikie pembe mahututi ya msimamo (yaani, pembe ya mwinuko zaidi ambayo mchanga unaweza kudumisha, ambapo iko karibu na kuanguka kwa sababu ya usumbufu mdogo) na shimo litabikishwe kwa chembe dogo tu[20]. Kwa kuchimba kwa mwendo wa parafujo wakati wa kutengeneza shimo lake kitukutuku hupunguza muda anaohitaji kukamilisha shimo[20].

Shimo linapokamilika, lava hutulia chini na kuzikwa katika mchanga na mataya tu yanayojitokeza juu ya uso, mara nyingi yakifunguka kabisa[21]. Rima lenye miteremko mikali ambao huelekeza mbuawa katika mdomo wa lava huku likiepuka maporomoko ya mchanga ni mojawapo ya marima rahisi na yenye ufanisi zaidi katika himaya ya wanyama[22]. Tabaka la chembe dogo huhakikisha kwamba maporomoko ya mchanga ambayo hubeba mbuawa ni makubwa iwezekanavyo[20]. Kwa kuwa pande za shimo zina mchanga mtifu kwa pembe yake ya msimamo[23], mdudu mdogo yeyote anayediriki kupita ukingo bila kukusudia, kama vile sisimizi, atateleza chini. Baada ya kuteleza hadi chini mbuawa hukamatwa mara moja na kitukutuku aoteaye. Akijaribu kukwea kuta zenye hila za shimo, anazuiwa haraka katika juhudi zake na kuletwa chini na mvua ya mchanga unaomtupiwa kutoka chini na lava[4]. Kwa kutupa mchanga kutoka chini ya shimo lava pia hudhoofisha pande za shimo na kuzisababisha kuanguka na kuleta mbuawa pamoja nazo. Kwa hivyo, haidhuru ikiwa lava hapigi mbuawa kwa mvua ya mchanga[21].

Rima katika mchanga lenye mabaki ya sisimizi.

Vitukutuku wanahitaji udongo mtifu, mara nyingi, lakini si lazima, mchanga. Wanaweza pia kumudu dutu ya chembe kubwa zaidi ambayo huchujwa nje ya udongo wakati wa kuchimba kwa shimo[20]. Lava hupendelea mahali pakavu palipolindwa dhidi ya mvua. Mara akitoka kwenye yai, lava mdogo hujilisha na wadudu wadogo sana, lakini kadiri anavyokua, huchimba mashimo makubwa zaidi ambayo hukamata mbuawa wakubwa, wakati mwingine wakubwa zaidi sana kuliko mwenyewe.[21]

Arithropodi wengine wanaweza kutumia uwezo wa kitukutuku kunasa mbuawa. Mabuu wa kipanga wa Australia Scaptia muscula (Diptera) anaishi katika marima ya vitukutuku, kama wale wa Myrmeleon pictifrons, na hula mbuawa waliokamatwa[24]. Na nyigu wa kike Lasiochalcidia igiliensis (Chalcididae, Hymenoptera) anajiruhusu kunaswa kimakusudi ili aweze kudusa kitukutuku kwa kutaga yai kati ya kichwa na thoraksi zake.[25]

Utafiti wa hivi karibuni umegundua kuwa vitukutuku mara nyingi "hucheza kuwa wamekufa" wanaposumbuliwa kwa muda tofauti tofauti (kutoka dakika chache hadi saa moja) ili kujificha kwa mbuai. Mbinu hii ni fanifu na inaweza kuongeza viwango vya kuishi kwa 20%[26]. Zaidi ya hayo, wanaonekana kuwa wameongeza manufaa yake, kwa sababu kuongeza zaidi muda hakuleti faida kubwa za kuishi kwa lava[27].

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Bankisus oculatus
  • Banyutus idoneus
  • Banyutus lethalis
  • Banyutus roseostigma
  • Banyutus shimba
  • Centroclisis benadirensis
  • Centroclisis brachygaster
  • Centroclisis mendosa
  • Centroclisis minor
  • Centroclisis somalina
  • Centroclisis taramassoi
  • Creoleon africanus
  • Creoleon diana
  • Creoleon ducalis
  • Creoleon falcatus
  • Creoleon limpidus
  • Creoleon mortifer
  • Creoleon nubifer
  • Cueta acuta
  • Cueta mysteriosa
  • Cueta obliqua
  • Cueta secreta
  • Cueta variegata
  • Cymothales bouvieri
  • Cymothales dulcis
  • Cymothales eccentros
  • Cymothales exilis
  • Cymothales johnstoni
  • Cymothales speciosus
  • Distoleon lanceipennis
  • Distoleon scolius
  • Distoleon somalica
  • Ganguilus pulchellus
  • Goniocercus klugi
  • Goniocercus similis
  • Hagenomyia lethifer
  • Hagenomyia tristis
  • Jaya dasymalla
  • Lachlathetes moestus
  • Macroleon formicarioides
  • Macroleon quinquemaculatus
  • Macronemurus lanthe
  • Macronemurus tinctus
  • Megistoleon ritsemae
  • Myrmeleon alluaudi
  • Myrmeleon doralice
  • Myrmeleon guttata
  • Myrmeleon obscurus
  • Myrmeleon picturatus
  • Nelebrachys aequatus
  • Nemoleon alcione
  • Nemoleon filiformis
  • Nemoleon iolanthe
  • Nemoleon lovenia
  • Neuroleon guttatus
  • Neuroleon lodwarinus
  • Neuroleon sansibaricus
  • Neuroleon striolus
  • Neuroleon torridus
  • Omoleon jeanneli
  • Palparellus rothschildi
  • Palpares aegrotus
  • Palpares digitatus
  • Palpares inclemens
  • Palpares nyicanus
  • Palpares obsoletus
  • Palpares papilionoides
  • Palpares torridus
  • Palpares tristis
  • Parapalpares somalicus
  • Pseudoformicaleo sordidatus
  • Pseudopalpares sparsus
  • Solter virgilii
  • Syngenes longicornis
  • Tomatares limonius
  1. https://www.antlionpit.com/afrotropical.html
  2. Swanson, Mark (2007). ""Antlion" in the World's Languages". The Antlion Pit. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Mares, Michael A. (1999). Encyclopedia of Deserts. University of Oklahoma Press. uk. 29. ISBN 978-0-8061-3146-7.
  4. 4.0 4.1 4.2 One or more of the preceding sentences incorporates text from a publication now in the public domain: Pocock, Reginald Innes (1911) "Ant-lion". In Chisholm, Hugh (ed.). Encyclopædia Britannica. Vol. 2 (11th ed.). Cambridge University Press. p. 147.
  5. Miller, Robert B.; Stange, Lionel A. (1 Novemba 2015). "Glenurus gratus (Say) (Insecta: Neuroptera: Myrmeleontidae)". Featured Creatures. University of Florida. Iliwekwa mnamo 22 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 6.2 Hawkeswood, Trevor J. (2006). "Effects of envenomation to a human finger and arm by the larva of an unidentified species of Myrmeleon (Neuroptera: Myrmeleontidae)" (PDF). Calodema. 7: 32–33. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-05.
  7. Nardi, James B. (2009). Life in the Soil: A Guide for Naturalists and Gardeners. University of Chicago Press. uk. 170. ISBN 978-0-226-56853-9.
  8. 8.0 8.1 Camp, Donya (2005). "Beneficials in the garden: Antlion". Galveston County Master Gardeners. Extension Horticulture at Texas A&M University. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. 9.0 9.1 Swanson, Mark (2007). "Antlion Larvae Behavior: Discarding the Body". The Antlion Pit. Iliwekwa mnamo 24 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. McEwen, P.K.; New, T.R.; Whittington, A.E. (2007). Lacewings in the Crop Environment. Cambridge University Press. uk. 4. ISBN 978-0-521-03729-7.
  11. Jervis, Mark A. (2007). Insects as Natural Enemies: A Practical Perspective. Springer Science & Business Media. uk. 28. ISBN 978-1-4020-6587-3.
  12. New, T. (1991). Insects as Predators. NSW University Press. uk. 69.
  13. 13.0 13.1 13.2 Swanson, Mark (2012). "Reproductive Behavior". The Antlion Pit. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. Swanson, Mark (2012). "Metamorphosis". The Antlion Pit. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Engel, Michael S.; Grimaldi, David A. (2007). "The neuropterid fauna of Dominican and Mexican amber (Neuropterida, Megaloptera, Neuroptera)" (PDF). American Museum Novitates (3587): 1–58. doi:10.1206/0003-0082(2007)3587[1:tnfoda]2.0.co;2. S2CID 49393365.
  16. Devetak, Dušan; Podlesnik, Jan; Janževocič, Franc (2014). "Antlion Dendroleon pantherinus (Fabricius, 1787) (Neuroptera: Myrmeleontidae) in Slovenia". Acta Entomologica Slovenica. 18 (2): 159–162.
  17. O'Neal, Matt. "Predatory insects" (PDF). MSU. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. Cocroft, Reginald Bifield (2014). Studying Vibrational Communication. Springer. uk. 319. ISBN 978-3-662-43607-3.
  19. Scharf, Inon; Ovadia, Ofer (2006). "Factors influencing site abandonment and site selection in a sit-and-wait Predator: A review of pit-building antlion Larvae" (PDF). Journal of Insect Behavior. 19 (2): 197–218. CiteSeerX 10.1.1.565.1350. doi:10.1007/s10905-006-9017-4. S2CID 36532488.
  20. 20.0 20.1 20.2 20.3 Franks, Nigel R.; Worley, Alan; Falkenberg, Max; Sendova-Franks, Ana B.; Christensen, K (2019). "Digging the optimum pit: antlions, spirals and spontaneous stratification". Proceedings of the Royal Society B: Biological Sciences. 286 (1899): 20190365. doi:10.1098/rspb.2019.0365. PMC 6452065. PMID 30900535.
  21. 21.0 21.1 21.2 Coelho, Joseph R. "The natural history and ecology of antlions (Neuroptera: Myrmeleontidae)". Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. Fertin, A. (2006). "Efficiency of antlion trap construction". Journal of Experimental Biology. 209 (18): 3510–3515. doi:10.1242/jeb.02401. PMID 16943491.
  23. Botz, Jason T.; Loudon, Catherine; Barger, J. Bradley; Olafsen, Jeffrey S.; Steeples, Don W. (2003). "Effects of slope and particle size on ant locomotion: Implications for choice of substrate by antlions". Journal of the Kansas Entomological Society. 76 (3): 426–435.
  24. Swanson, Mark (2007). "What are Antlions?". The Antlion Pit. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  25. Piek, Tom (2013). Venoms of the Hymenoptera: Biochemical, Pharmacological and Behavioural Aspects. Elsevier. uk. 74. ISBN 978-1-4832-6370-0.
  26. Giaimo, Cara. "The Power of Playing Dead", The New York Times, 2021-03-07. (en-US) 
  27. Franks, Nigel R.; Worley, Alan; Sendova-Franks, Ana B. (2021). "Hide-and-seek strategies and post-contact immobility". Biology Letters. 17 (3): 20200892. doi:10.1098/rsbl.2020.0892. PMC 8086978. PMID 33653098.