Plau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Trekta inavuta plau yenye ulimi 5; ardhi nyuma ya plau imegeuzwa
Plau sahili huko Misri mnamo 1200 KK; aina hii bado inatumiwa katika nchi kadhaa

Plau (kut. Kiing. plough (UK) au plow (US)) ni mashine sahili ya kulimia ardhi kwenye kilimo.

Plau huvutwa shambani kwa nguvu ya trekta au mashine, mnyama au pia ya kibinadamu. Ulimi wa plau unakata ardhi na kuigeuza. Kwa njia hii ardhi inalainishwa na tabaka za chini zenye lishe mpya ya mimea zinapelekwa juu. Vilevile majani yasiyotakiwa yanachimbwa chini ya ardhi hivyo kuipa nafasi mimea mipya kutokana na mbegu unaopandwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Plau kwa jumla imechukua nafasi ya kilimo kwa jembe. Plau za kwanza zilikuwa tu miti yenye tawi la kando lililofanya kazi ya ulimi wa baadaye.

Baadaye zimetenegenzwa kwa ubao tu na ulimi wa fimbo kali ulivuta mistari ya makuo kwa ajili ya mbegu kwenye ardhi.

Watu waliendelea kuongeza jembe la chuma kwenye ncha ya ulimi hivyo kuifanya plau ya kudumu zaidi hate penye ardhi gumu.

Baadaye ulimu ulipanushwa na kupokea umbo lililorudisha ardhi kando la mstari wa makuo. Tangu kupatikana kwa matrekta plau ziliongezeka ulimi.

Siku hizi plau kubwa huwa na gurudumu ya kisu mahali pa ulimi.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Plau kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: