Taya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Taya ya chini ya binadamu

Taya ni sehemu ya muundo wa kinywa wa wanyama wengi wenye kazi ya kushika na kuhamisha chakula mara nyingi pamoja na kukikatakata.

Mataya ya vertebrata[hariri | hariri chanzo]

Kwenye vertebrata au wanyama wenye uti wa mgongo mataya yanajengwa kwa mfupa au gegedu na kupatikana kwa jozi yaani taya la chini na taya la juu. Kwa spishi nyingi huwa na meno.

Kwenye wanyama wenye miguu minne mifupa ya taya la juu imeunganishwa na mifupa ya fuvu ya ubongo. Taya la chini linaunganishwa kwa njia mbalimbali na taya la juu. Nyoka zinaweza kuachana mataya yote mawili kabisa na hivyo kumeza hata windo kubwa sana.

Kwenye mamalia taya la chini hushikwa kwa kiungo imara na taya la juu na mfumo huu unaweka mipaka kwa uwezo wa kufungua kinywa.

Mataya ya arithropodi[hariri | hariri chanzo]

Mataya ya kando ya sisimizi

Kwenye arithropodi kama wadudu mataya yako kando ya kinywa na yamejengwa kwa chitini. Yanashika chakula pia wanyama wadogo wengine wanaowindwa na kukipasua.

Gray188.png Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Taya kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.