Daktari wa meno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daktari wa meno anapiga sindano kinywani kabla ya kuendelea na tiba

Daktari wa meno ni tabibu aliyesoma uganga wa meno hasa. Anahusika na utambuzi, kinga na tiba ya magonjwa kinywani, si meno pekee.

Katika nchi nyingi za dunia daktari huyu anapaswa kusoma kwenye chuo kikuu angalau hadi kiwango wa bachelor. Nchi nyingine zinatambua pia masomo kwenye vyuo vya pekee visivyofikia kiwango hiki.

Masomo yako pamoja na tiba kwa jumla maana misingi ya elimu ya mwili, magonjwa na madawa ni sawa kwa matabibu wa kila aina.

Daktari wa meno anatakiwa kujua hasa kazi ya mkononi ya kushughulika vifaa vya kiganga kwa ajili ya kutoboa na kujaza meno.

Baada ya masomo ya kimsingi daktari wa meno anaweza kuendelea kusoma na kuwa bingwa katika fani kama mpasuaji wa meno, mpasuaji wa taya, redioloji ya meno, ushauri wa afya ya meno ya umma na mengine.