Nenda kwa yaliyomo

Elizabeti wa Hungaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Elizabeth wa Hungaria kadiri ya msanii wa Bavaria (1520 hivi), Musée de l’Œuvre Notre-Dame, Strasbourg (Ufaransa).
Mt. Elizabeti akifuma kwa ajili ya fukara.

Elisabeti wa Hungaria (kwa Kijerumani Elisabeth von Thüringen, kwa Kihungaria Árpád-házi Erzsébet; Pressburg, leo Bratislava, Slovakia, au ngome ya Sárospatak, Hungaria[1][2][3], 7 Julai 1207 - Marburg, Ujerumani, 17 Novemba 1231) alikuwa malkia mdogo wa Thuringia kutoka Ufalme wa Hungaria[4].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Walutheri na Waanglikana kama mtakatifu.[5]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Novemba[6].

Alikuwa binti wa Andrea II wa Hungaria na Getrude wa Merania.

Aliishi Pressburg hadi umri wa miaka 4, alipopelekwa kwenye ikulu ya Thuringia (Ujerumani wa kati), ajiandae kuolewa na mtoto wa mfalme mdogo wa huko ili kuimarisha agano kati ya nchi hizo mbili.

Elizabeti aliolewa na Ludwig IV wa Thuringia akiwa na umri wa miaka 14, akamzalia watoto watatu.

Mwaka 1223 Wafransisko walifika nchini wakamuathiri Elisabeti, lakini Ludwig hakuchukizwa na juhudi za mke wake. Ndoa yao iliendelea vizuri hadi mwisho.

Wakati huo padri Konrad wa Marburg alipata kuwa muungamishi wake.

Mwanzo wa mwaka 1226, mafuriko, njaa na maradhi vilipoathiri Thuringia, Ludwig alikwenda Cremona (Italia) kwa kikao cha bunge la Dola Takatifu la Kiroma kama mwakilishi wa Kaizari Frederick II. Elizabeti alishika uongozi wa nchi akisaidia kwa ukarimu watu wote wenye shida. Alijenga pia hospitali chini ya ikulu akahudumia mwenyewe waliopokewa huko.

Maisha ya Elizabeti yalibadilika kabisa tarehe 11 Septemba 1227 kutokana na kifo cha Ludwig, akiwa safarini Otranto, kwenda kujiunga na Vita vya msalaba. Hivyo Elizabeti akabaki mjane akiwa na miaka 20 tu. Alipopata habari, alisema, "Amekufa. Amekufa. Kwangu ni kama kwamba ulimwengu wote umekufa."[7]

Hapo shemeji yake, Heinrich Raspe wa Thuringia alishika uongozi kwa niaba ya mtoto wa kwanza wa Elizabeti, Hermann II wa Thuringia (12221241).

Baada ya mabishano makali kuhusu mahari aliyojiletea, ambayo Konrad wa Marburg aliteuliwa na Papa Gregori IX amtetee, pamoja na tabu nyingine kubwa, ambazo Elizabeti alizivumilia kishujaa, aliacha ikulu ya Wartburg, aliwagawia fukara mali yake, akahamia Marburg huko Hesse, alipojenga hospitali nyingine na kuhudumia maskini[8].

Huko Elizabeti, aliyekwishazoea tangu muda mrefu kutafakari mambo ya mbinguni, alimwekwea Konrad nadhiri kuu kama za kitawa, akaishi kifukara na kijumuia na wanawake wachache wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko wa Asizi.

Konrad alimtendea kwa ukali sana, akimlazimisha kuachana na watoto wake.

Ingawa ndugu yake, askofu Ekbert wa Bamberg, alitaka kumlazimisha aolewe tena, Elizabeti alikataa katakata [9], akawa kielelezo cha matendo ya huruma hadi kifo chake alipokuwa na miaka 24 tu.

Sala yake

[hariri | hariri chanzo]

Bwana, ukitaka kuwa pamoja nami, mimi nataka kuwa pamoja nawe, nisitake kutengana nawe kamwe.

Kanisa la Mt. Elizabeti huko Marburg
Ramani ya kanisa hilo

Mapema baada ya kifo chake, miujiza iliripotiwa kutokea kaburini pake. Kwa pendekezo la Konrad, na agizo la Papa, kesi ilianza kati ya walioponywa kiajabu kati ya Agosti 1232 na Januari 1235.

Matokeo ya uchunguzi huo yaliambatanishwa na kitabu kifupi kuhusu maisha yake, na shuhuda za wenzake (Libellus de dictis quatuor ancillarum s. Elisabeth confectus).

Basi, Elizabeti alionekana kustahili atangazwe haraka na Papa Gregori IX kuwa mtakatifu 27 Mai 1235 huko Perugia.

Baadaye vitabu vingi viliandikwa juu yake, maarufu kati ya hivyo ni kile cha Dietrich wa Apolda, Vita S. Elisabeth, kilichoandikwa kati ya miaka 1289 na 1297.

Patakatifu pa Elizabeti pakawa mahali pa hija hasa katika karne ya 15.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Albrecht, Thorsten (2007). Elisabeth von Thüringen: Leben und Wirkung in Kunst und Kulturgeschichte. Petersberg: Michael Imhof Verlag. uk. 7. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  2. Ohler, Norbert (2006). Elisabeth von Thüringen: Fürstin im Dienst der Niedrigsten. Gleichen: Muster-Schmidt Verlag. uk. 15. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  3. Zippert, Christian (2007). Hingabe und Heiterkeit: Vom Leben und Wirken der heiligen Elisabeth. Kassel: Verlag Evangelischer Medienverband. uk. 9. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help), 2007), 9.
  4. Catholic Encyclopedia "St. Elizabeth of Hungary". Catholic Encyclopedia. http://www.newadvent.org/cathen/05389a.htm Catholic Encyclopedia.
  5. "Saint Elizabeth of Hungary". Encyclopædia Britannica. http://www.britannica.com/EBchecked/topic/184889/Saint-Elizabeth-of-Hungary.
  6. Martyrologium Romanum
  7. Rainer Koessling, ed. and trans., Leben und Legende der heiligen Elisabeth nach Dietrich von Apolda (Frankfurt am Main: Insel Verlag, 1997), 52.
  8. https://www.santiebeati.it/dettaglio/25150
  9. Rainer Koessling, ed. and trans., Leben und Legende der heiligen Elisabeth nach Dietrich von Apolda (Frankfurt am Main: Insel Verlag, 1997), 59.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.