True Jesus Church

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

True Jesus Church ni kanisa dogo lililoanzishwa Uchina mwaka 1917. Asili yake ni katika mwelekeo wa Kipentekoste ndani ya Ukristo.

Inadaiwa ya kwamba TJC lina Wakristo milioni 1.5 katika nchi 45. Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo. Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo mnamo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru", wengi wao wakiwa na asili ya Kichina. Tangu mwaka 2002 TJC lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nalo mnamo mwaka 2004.

TJC linashika imani mbalimbali za pekee zinazotofautisha kikundi hiki na madhehebu mengine ya Kikristo.

Kimsingi wanaamini ya kwamba wenyewe ni kanisa pekee la kweli la Kristo; makanisa mengine yote ni ya uwongo.

Wanajieleza kwamba Yesu Kristo alianzisha Kanisa moja la kimitume lililopeleka Injili katika nchi mbalimbali. Lakini Kanisa hilo likavurugika na kupatwa na imani potovu na uzushi hadi mwaka 1917 Mungu alipoamua kulifufua kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na ndio mwanzo wa TJC.

Kati ya imani nyingine za pekee ni hizi zifuatazo:

  • atakayebatizwa lazima akubali TJC ni Mwili wa Kristo.
  • Wakanusha mafundisho ya Utatu wa Mungu wakisema "Yesu yu Mungu wa kweli".
  • Wanakataza ibada za Jumapili wakidai siku ya Jumamosi ndiyo siku takatifu ya Sabato iliyoamriwa na Mungu.
  • Hawasheherekei sikukuu za Krismasi na Pasaka kwa sababu wanaamini zina asili za kipagani na ni mifano ya imani ya Kikristo ya asili kuingiliwa na uzushi.
  • Wanaangalia desturi ya kuosha miguu kama sakramenti iliyoamriwa na Yesu.

Mafundisho mengine yanafanana na yale ya Wapentekoste wengine, kama vile kusema kwa lugha za roho au kubatizwa kwa jina la Yesu kwa kuzamishwa chini ya maji, tena maji ya kutiririka.

TJC ni kati ya vikundi vinavyojitahidi sana kusambaza habari zao kupitia tovuti.

Wamefaulu kuingiza habari zao katika Wikipedia za lugha 230 lakini mara nyingi makala hizo ni tafsiri tu ya maelezo waliyoyaandaa wenyewe. Ingefaa yajadiliwe na watu wengine.

Kwa mfano, ingefaa ieleweke ukweli wa msimamo wa TJC kulingana na Biblia wanapodai kwa miaka mia kadhaa duniani halikuwepo tena Kanisa la kweli. Mbona Yesu aliahidi, "Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20)? Tena "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18).

[hariri] Imani kuu kumi za kanisa ni:

  1. Roho Mtakatifu: "kupatwa na Roho Mtakatifu ambayo huthibitishwa na uwezo wa kuongea pepo, ni hakikisho yetu ya kurithi ufalme mbinguni."
  2. Ubatizo: "Kubatizwa kwa maji ni sakramenti ya kutubu dhambi na kuzaliwa tena. Ubatizo unafaa kufanywa kwenye maji ya kawaida kama vile kwenye mto, kisima au ziwa. Mbatizaji, ambaye pia amebatizwa vilevile na kwa Roho Mtakatifu, hutimiliza ubatizaji kwa jina la Mwana Yesu Kristu. Kichwa cha Mbatizwaji hutumbUkizwa kwenya maji kukamilisha ubatizo."
  3. Kutakaswa: "Sakramenti ya kunawa miguu huwezesha binafsi kuwa na shirika na Bwana Yesu. Pia hutukumbusha mara kwa mara ni lazima tuwe na upendo, utakatifu, unyeyekevu, msamaha na utumishi. Yeyote aliyepata ubatizo wa maji ni lazima aoshwe miguu kwa jina la Yesu Kristo. Kunawishwa miguu yaweza kufanywa inapohitajika."
  4. Komunio Takatifu: "Komunio Takatifu ni sakramenti ya kusheherekea kifo cha Mola Yesu Kristu. Inatueneza kupata mwili na damu ya mwokozi wetu na kuwa na umoja naye ili tuweze kupata uzima wa milele na kufufuliwa siku ya mwisho. Sakramenti hii ina haja ya kufanywa kila iwezekanapo. Katika sakramenti hii hutumiwa mkate na divai."
  5. Sabato: "Siku ya sabato, ambayo ni siku ya saba kwenye wiki (Jumamosi), ni siku takatifu, iliyobarikiwa na kusahihishwa na Mungu Baba. Siku hii hubudiwa kwa ajili ya ukumbusho wa maumbo na pia ukombozi na Mungu Baba, na tarajio la pumziko la milele daima kwenye maisha yatakayokuja."
  6. Yesu Kristo: "Yesu Kristo, Neno aliyefanyika mwili, akafa msalabani kwa msamaha wa wenye dhambi, akafufuka siku ya tatu akapaa juu mbinguni. Yeye ndiye mwokozi wa binadamu, Muumba wa mbingu na nchi na ndiye Mungu wa kweli."
  7. Biblia Takatifu (Maandiko Matakatifu): "Biblia Takatifu, ina Agano la Kale na Agano Jipya ambayo imewezeshwa na Mungu na yenye Maandiko Matakatifu ya kweli kwa maisha ya Mkristo."
  8. Wokovu: "Wokovu unatolewa kwa neema ya Mungu kupitia imani. Waaminio lazima wamwamini Roho Mtakatifu ili kupata utakatifu, kwa kumheshimu Mungu, na kwa upendo wa watu"
  9. Kanisa: "Kanisa, lililetwa na Bwana Yesu Kristo, kupitia Roho Mtakatifu kipindi cha 'nyakati za mwisho', ni kanisa la kweli lililorejeshwa nyakati za ki'Apostoliki."
  10. Hukumu ya mwisho: "Kuja kwa Yesu kwa mara ya pili itakuwa siku ya mwisho wakati akishuka kutoka mbinguni kuhukumu: walio na haki watapokea uzima wa milele wasio na haki watahukumiwa milele"
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine