Vita za Misalaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mwanajeshi wa misalaba (uchoraji wa karne ya 13)

Vita za Misalaba (pia: vita vya msalaba) vilitokea kati ya mataifa ya Wakristo wa Ulaya na watawala Waislamu wa nchi za Mashariki ya Kati wakati wa karne za 11 hadi 13, hasa kuanzia 1095 hadi 1291 katika jina la dini na kwa baraka za Kanisa Katoliki.

Kwa maana nyingine na pana zaidi "vita vya msalaba" vilikuwa jitihada za watawala Ulaya kutetea haki za Wakristo wenzao wa nchi hizo, au kujitetea kwa silaha na vita na wakati huohuo kueneza himaya yao pamoja na dini ya Kikristo .

Jina limetokana na desturi ya wanajeshi wa vita ya kwanza ya misalaba kushona alama ya msalaba juu ya nguo zao kama dalili ya kiapo walichotoa kuwafukuza Waislamu katika mji wa Yerusalemu.

Mtawa Peter akihubiri vita ya msalaba mbele ya makabaila wa Ufaransa

Chanzo cha vita za misalaba[hariri | hariri chanzo]

Hali ya Wakristo wa Yeruaslemu na Mashariki ya Kati[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 637 BK mji wa Yerusalemu pamoja na nchi ya Palestina ilikuwa mkononi mwa Waarabu Waislamu waliofaulu kushinda jeshi la Bizanti. Wakazi wengi wa nchi waliendelea kufuata dini zao hasa Ukristo na Uyahudi, lakini sehemu ya wananchi polepole waligeukia pia Uislamu.

Yerusalemu iliendelea kuwa lengo la wahiji Wakristo waliotaka kutembelea mahali ambako [[Yesu Kristo[[ aliishi hasa Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu.

Watawala Waarabu waliwahi kuahidi kuheshimu Wakristo walioishi chini ya utawala wao na kutunza haki zao.

Hali hiyo ilibadilika vibaya mara ya kwanza wakati ya khalifa Al Hakim wa Misri aliyeanza kuwatesa Wakristo kuanzia mwaka 1001; Kanisa la Kaburi na Ufufuo lilibomolewa pamoja na makanisa mengi nchini Palestina. Dhuluma ya Al Hakim ililegezwa na wafuasi wake, na kanisa la Yerusalemu likajengwa upya kwa msaada wa Kaisari wa Bizanti.

Amani katika mashariki ya kati ilivurugika tena kutokana na uenezaji wa Waseljuki waliokuwa kabila kubwa la Waturuki kutoka Asia ya kati waliokuwa wamehamia magharibi, kupokea Uislamu na kutawala Uajemi pamoja na maeneo ya jirani. Mwaka 1071 jeshi la Waseljuki lilishinda Wabizanti kwenye mapigano ya Manzikert na kutwaa sehemu kubwa ya Anatolia pamoja na Siria na Palestina. Vikosi vya Seljuki walishambulia pia mara kwa mara wahiji Wakristo kutoka Ulaya walioelekea kaburi takatifu mjini Yerusalemu na hija ya kikristo ya Yerusalemu ikaona kipindi kigumu.

Mnamo mwaka 1095 Kaisari Aleksios I wa Bizanti alipanga kuwaondoa tena Waseljuki katika Anatolia kutoka sehemu walizowahi kutwaa miaka michache ya nyuma. Hapa alituma mabalozi kwa Papa Urban II wa Roma kwa kusudi la kupata msaada wa askari wa kukodiwa kutoka Ulaya. Alifanya hivyo miaka 40 baada ya kutokea kwa farakano la mashariki mwaka 1054 kati ya makanisa ya Waorthodoksi na Roma, labda kwa tumaini la kuanzisha maelewano upya.

Wito la Papa Urban II mwaka 1095[hariri | hariri chanzo]

Papa Urban II aliwapokea mabalozi wa Bizanti katika Italia akasikia ombi la Kaisari. Inaonekana aliona nafasi ya kuwaelekeza mashariki makabaila wadogo wa Ulaya ambao walizoea kuvuruga amani ya Ulaya kwa mapigano ya mfululizo na vita ndogondogo, wakiharibu mali ya watu wengi. Kwenye sinodi ya Clermont mbele ya maaskofu na maabate wa Ufaransa alitangaza ombi la msaada kutoka Bizanti na kuhimiza wakabaila kupokea wito huu na kuwasaidia Wakristo wenzao wa mashariki badala ya kuharibu mali ya watu wa nyumbani. Hotuba ya Papa ikapokewa na sinodi na umati mkubwa wa wasikilizaji walioanza kuita kwa sauti moja "Mungu anaitaka" (Deus lo vult).

Makabaila kadhaa walipiga magoti mbele ya Papa wakiomba baraka kwa mipango yao ya kuitikia wito wake. Wengine walisikia habari hizi baadaye, na makabaila wengi wa Ufaransa waliamua kujiunga na mradi wa kwenda mashariki kuwasaidia Wakristo wa huko na kuwaondoa Waislamu katika nchi zilizowahi kuwa nchi za Kikristo.

Wahubiri walizunguka Ulaya kutangaza mpango huo. Ni wahubiri hao waliosambaza ujumbe wa kwamba shabaha la vita ni Yerusalemu, ingawa wala Kaisari Aleksios wala Papa Urban waliwahi kutumia jina hili. Lakini wakati ambako watu wengi hawakujua kusoma na kuandika wala hawakuwahi kuona ramani jina la Yerusalemu lilijulikana kote hata kama wasikilizaji wengine hawakuelewa tofauti kati ya mahali pa kidunia na Yerusalemu wa mbinguni iliyohubiriwa pia kanisani.

Vita ya kwanza ya misalaba[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1096 vilikusanyika vikundi vya watu wa kawaida walioongozwa na wahubiri waliotaka kwenda mashariki kwa hiari yao, ingawa si wanajeshi. Umati huo waliomba na kutisha miji walipopita wapewe chakula na misaada kwa sababu wengi hawakuwa na kitu wenyewe. Katika miji ya Ujerumani ya Magharibi na kusini walianza kushambulia Wayahudi walioishi huko na kuwaua wengi.

(inaendelea)


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • Crusade Siege Siege of a Mohammedan fortification during the crusades