Jimbo Katoliki la Eldoret
Mandhari
Jimbo Katoliki la Eldoret ni mojawapo kati ya majimbo 27 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.
Liko chini ya jimbo kuu la Kisumu.
Tarehe 10 Julai 2025 limegawanywa ili kuanzisha Jimbo Katoliki la Kapsabet katika kaunti ya Nandi. Tangu hapo limebaki na Km2 6,365.6, wanapoishi watu 1,619,666, ambao kati yao Wakatoliki ni 581,345.
Parokia ni 65, mapadri ni 112, wakiwemo wanajimbo 92, mashemasi ni 8, watawa wa kiume ni 31 na wa kike ni 211, waseminari ni 55 na makatekista 605.
![]() |
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Eldoret kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |