Guinea ya Ikweta
Jamhuri ya Gine ya Ikweta | |
---|---|
República de Guinea Ecuatorial (Kihispania) République de Guinée équatoriale (Kifaransa) República da Guiné Equatorial (Kireno) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unidad, Paz, Justicia (Kihispania) "Umoja, Amani, Haki" | |
Wimbo wa taifa: Caminemos pisando las sendas de nuestra inmensa felicidad (Kihispania) "Tutembee tukifuata njia za furaha yetu kubwa" | |
Mahali pa Guinea ya Ikweta | |
Ramani ya Guinea ya Ikweta | |
Mji mkuu | Malabo |
Mji mkubwa nchini | Bata |
Lugha rasmi | Kihispania Kifaransa Kireno |
Serikali | Udikteta |
• Rais | Teodoro Obiang |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 28 050[1] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 1 737 695[1] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 10.041[2] |
• Kwa kila mtu | USD 6 502[2] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 28.356[2] |
• Kwa kila mtu | USD 18 362[2] |
Maendeleo (2021) | 0.596[3] - wastani |
Sarafu | Faranga ya CFA |
Majira ya saa | UTC+1 |
Msimbo wa simu | +240 |
Msimbo wa ISO 3166 | GQ |
Jina la kikoa | .gq |
Gine ya Ikweta (pia: Ginekweta au Guinea ya Ikweta), kirasmi Jamhuri ya Gine ya Ikweta, ni nchi mojawapo ndogo ya Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati.
Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Gine upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ghuba ya Guinea na Ikweta.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Nchi ina sehemu mbili kuu. Eneo kubwa liko kwenye bara la Afrika katika kanda ya Rio Muni. Ndipo walipo wakazi wengi zaidi.
Sehemu iliyoendelea zaidi, pamoja na mji mkuu, iko kwenye kisiwa cha Bioko. Pamoja na visiwa vingine, hasa Annobon, hiyo kanda ya Visiwa ni sehemu ya pili ya nchi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Poo) ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela).
Siasa
[hariri | hariri chanzo]Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Mikoa
[hariri | hariri chanzo]Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 8 iliyopo katika kanda mbili:
- Mkoa wa Annobón (mji mkuu wa mkoa: San Antonio de Palé)
- Mkoa wa Bioko Norte (Malabo)
- Mkoa wa Bioko Sur (Luba)
- Mkoa wa Centro Sur (Evinayong)
- Mkoa wa Kié-Ntem (Ebebiyín)
- mkoa wa Litoral (Bata)
- Mkoa wa Wele-Nzas (Mongomo)
- Mkoa wa Djibloho (Ciudad de la Paz)
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wananchi wengi (80%) ni wa kabila la Wafang, ambao ni wa Kibantu.
Lugha
[hariri | hariri chanzo]Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi isiyotambulika kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi.
Dini
[hariri | hariri chanzo]Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (88%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika na Baha'i ni 5%. Waislamu ni 2%.
Utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Equatorial Guinea". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 28 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (GQ)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 19 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Human Development Report 2021/2022" (PDF) (kwa Kiingereza). United Nations Development Programme. 8 Septemba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-10-09. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
- Max Liniger-Goumaz, Udogo siyo urembo : Hadithi ya Guinea ya ikweta (French 1986, translated 1989) ISBN 0-389-20861-2
- Ibrahim K. Sundiata, Equatorial Guinea: Colonialism, State Terror, and the Search for Stability (1990, Boulder: Westview Press) ISBN 0-8133-0429-6
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 5 Mei 2009 kwenye Wayback Machine. (Kihispania), (Kiingereza)
- makala maalum ya serikali ya Guinea ya Ikweta Ilihifadhiwa 22 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- makala ya Elimu Guinea ya ikweta
- makala ya wanasiasa wa upinzani Ilihifadhiwa 1 Septemba 2005 kwenye Wayback Machine.
Habari
[hariri | hariri chanzo]- allAfrica - Equatorial Guinea taarifa ya habari
Uchambuzi na Maelekezo
[hariri | hariri chanzo]- BBC News Country Profile - Guinea ya ikweta
- CIA World Factbook - Equatorial Guinea Ilihifadhiwa 27 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- Open Directory Project - Equatorial Guinea maelekezo
- Stanford University – Afrika kusini mwa Sahara: Guinea ya ikweta Maelekezo
- Guinea ya ikweta, Afrika - Ikweta-Guinea Ilihifadhiwa 12 Agosti 2004 kwenye Wayback Machine.
- Chuo kikuu cha Pennsylvania - African Studies Center: Ikweta-Guinea Maelekezo
- Yahoo! - Guinea ya ikweta Ilihifadhiwa 21 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. maelekezo
Koo na Makabila
[hariri | hariri chanzo]- African Pygmies (Utamaduni na mziki wa watu wa Guinea ya ikwete / picha na ukoo.)
Utalii
[hariri | hariri chanzo]- Equatorial Guinea travel guide kutoka Wikisafiri
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]- Sahuri za benki, Guinea ya ikweta, from the Fair Finance Watch
- (Uhifadhi wa biashara, guinea ya ikweta) nchini Hispania Ilihifadhiwa 24 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea ya Ikweta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |