São Tomé na Príncipe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
|
|||||
| Wito la taifa: Hija hifadhiwa | |||||
| Wimbo wa taifa: Independência total (Kireno Uhuru kamili) |
|||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | São Tomé |
||||
| Mji mkubwa nchini | São Tomé | ||||
| Lugha rasmi | Kireno | ||||
| Serikali | Jamhuri Fradique de Menezes Tomé Vera Cruz |
||||
| Uhuru - Date |
Kutoka Ureno 12 Julai 1975 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
964 km² (169) 0% (kisiwa) |
||||
| Idadi ya watu - 2005 kadirio - ? sensa - Msongamano wa watu |
169,000 (173) haiko 171/km² () |
||||
| Fedha | Dobra (STD) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+0) (UTC) |
||||
| Intaneti TLD | .st | ||||
| Kodi ya simu | +239 |
||||
Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe ni nchi ya kisiwani ndogo katika Guba ya Guinea mbele ya mwambao wa Afrika ya Magharibi. Yenyewe ina visiwa viwili vikubwa vya São Tomé na Príncipe pamoja na visiwa vidogo-vidogo. Visiwa hivi viwili vina umbali kati yao wa kilomita 140 viko takriban kilomita 250 kutoka pwani la Gabon.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Visiwa vyote vya nchi ni vilele vya milima ambayo ni sehemu ya safu za volkeno zilizokua kuanzia msingi wa bahari hadi kufikia usoni. Volkeno hizi si hai tena.
São Tomé ni kisiwa kikubwa chenye takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi. Kisiwa kina urefu wa rasi 48 km na upana wa 32 km. Kimo cha milima yake hufikia 2,024 m juu ya UB. Jina la Sao Tome limetolewa na Wareno waliofikia kisiwani siku ya mtakatifu Thomas katika kalenda ya kanisa katoliki.
Kisiwa cha pili Príncipe kina urefu wa 16 km na upana wa 6 km. Milima yake hufikia 927 m juu ya UB.
Rolas ni kisiwa kidogo kusini ya Sao Tome chenye wakazi 200 na mstari wa ikweta unapitia humo.
[hariri] Historia
[hariri] Siasa
[hariri] Utawala
Nchi ina mikoa miwili inayolingana na visiwa viwili na wilaya saba. Wilaya sita ziko kwenye kisiwa kikubwa cha Sao Tome na ya saba iko Principe.
Nchi ilifuata siasa ya chama kimoja tangu uhuru hadi 1990. Katiba ya 1990 imeruhusu vyama vingi. Rais huchaguliwa na wananchi wote kwa muda wa miaka mitano.
Uchaguzi wa 26 Machi 2006 ulileta bunge kama lifuatalo:
- MDFM/PCD (Movimento Democrático Força da Mudança / Partido da Convergência Democrática) - wabunge 23
- MLSTP-PSD (Movimento de Libertação - Partido Social Democrata) - wabunge 20
- ADI (Acção Democrática Independente) - wabunge 11
- MNR (Movimento Novo Rumo) - mbunge 1
[hariri] Jiografia
[hariri] Uchumi
[hariri] Watu na ukoo
[hariri] Utamaduni
[hariri] Viungo vya Nje
[hariri] Serikali
- Presidência da República Democrática de São Tomé e Príncipe - Jamhuri ya kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe (makala rasmi, Ureno)
- Assembleia Nacional de São Tomé e Príncipe -Baraza la Taifa ya São Tomé na Príncipe (makala rasmi, kireno)
- Instituto Nacional de Estatística - Chuo cha Taifa cha statistikia (kireno)
- São Tomé and Príncipe Government & Political Resources Page
[hariri] Habari
[hariri] Uchambuzi
- BBC News - Country Profile: Sao Tome na Principe
- (kitabu cha wadadisi wa Marekani) - Sao Tome na Principe
- kufungua muundo wa maelekezo - Sao Tome na Principe maelekezo
[hariri] Utalii
- {{{2}}} travel guide kutoka Wikisafiri
Agensia ya Usafiri (wenyeji) Navetur-Equatour [1]
[hariri] Mazingira
[hariri] Mambo mengine
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |


