Nenda kwa yaliyomo

Ndege (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndege (Aves)
Ndege (Buabua-kishungi mkubwa)
Ndege (Buabua-kishungi mkubwa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli ya juu: Tetrapoda
(bila tabaka): Dinosauria
(bila tabaka): Theropoda
Ngeli: Aves (Ndege)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nusungeli na oda za juu:

Miguu, midomo na utumbo wa ndege

Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo (chordata) na miguu miwili wanaozaliana kwa kutaga mayai.

Biolojia inawapanga katika ngeli ya Aves.

Ndege wameenea kote duniani kuanzia Aktiki hadi Antaktiki.

Ndege mdogo huwa na sentimita 5 tu na ndege mkubwa ana urefu wa mita mbili na nusu.

Ndege huwa na manyoya, mdomo bila meno, mayai yenye ganda gumu, moyo wenye vyumba vinne na mifupa myepesi ambayo ni imara.

Ndege walio wengi wana uwezo wa kuruka hewani na maumbile yao yanalingana na kusafiri hewani. Ila tu aina chache zimepoteza uwezo wa kuruka kwa mfano mbuni, ngwini na ndege kadhaa wa visiwani.

Aina nyingi za ndege huwa na misafara ya kila mwaka, kwa mfano korongo mweupe husafiri kila mwaka kati ya Afrika na Ulaya.

Uainishaji

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndege (mnyama) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.