Ninga-bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ninga-bahari
Ninga-bahari wa Wilson
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Procellariiformes (Ndege kama walinzi)
Familia: Hydrobatidae (Ninga-bahari)
Jenasi: Nusufamilia Hydrobatinae

Hydrobates Boie, 1822
Oceanodroma Reichenbach, 1853
Nusufamilia Oceanitinae
Fregetta Bonaparte, 1855
Garrodia W.A. Forbes, 1881
Nesofregetta Mathews, 1912
Oceanites Keyserling & J.H. Blasius, 1840
Pelagodroma Reichenbach, 1853

Ninga-bahari ni ndege wa familia Hydrobatidae. Wana mnasaba na walinzi lakini ni wadogo kuliko hawa. Familia hii ina nusufamilia mbili (tazama sanduku la uainishaji), lakini utafiti mpya wa ADN umeonyesha kama ingefaa zaidi kuzichukulia kama familia kamili. Spishi za Hydrobatinae ni weusi au kijivucheusi na weupe kwa kiasi mbalimbali. Spishi za Oceanitinae ni weusi juu na weupe chini. Huruka kwa kupapatika. Hula gegereka wa planktoni na samaki wadogo wakiangama hewani na kukanyaga maji.

Kwa kawaida ninga-bahari huzaa kwa visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia ndege au wanyama mbua. Jike hulitaga yai moja tu kwa kawaida ndani ya kishimo au mwanya wa mwamba.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]