Mlinzi mzamaji
Mandhari
Mlinzi mzamaji | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mlinzi mzamaji mdogo (Pelecanoides urinatrix)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Walinzi wazamaji ni ndege wadogo wa bahari wa jenasi Pelecanoides, jenasi pekee ya familia Pelecanoididae. Wataalamu wengine huwaainisha katika familia Procellariidae (walinzi), lakini walinzi wazamaji ni wadogo kuliko walinzi wengine, wana mabawa mafupi na mirija ya pua inaelekea juu badala ya mbele. Wanatokea bahari za kusini na huzamia kabisa ili kuwakamata gegereka wadogo hasa (krili, kopepodi na amfipodi) na samaki na ngisi wadogo pia. Majike hulitaga yai moja tu ardhini katika makoloni kwenye visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kwa kawaida huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia shakwe-waporaji.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Pelecanoides georgicus, Mlinzi Mzamaji wa Georgia Kusini (South Georgia Diving Petrel)
- Pelecanoides urinatrix, Mlinzi Mzamaji Mdogo (Common Diving Petrel)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Pelecanoides garnotii (Peruvian Diving Petrel)
- Pelecanoides magellani (Magellan Diving Petrel)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mlinzi mzamaji wa Georgia Kusini
-
Peuvian diving petrel