Korongo (Ciconiidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Korongo
Korongo domo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Ciconiiformes (Ndege kama makorongo)
Familia: Ciconiidae (Ndege walio na mnasaba na makorongo)
Gray, 1840
Jenasi: Anastomus Bonnaterre, 1791

Ciconia Brisson, 1760
Ephippiorhynchus Bonaparte, 1855
Jabiru Hellmayr, 1906
Leptoptilos Lesson, 1831
Mycteria Linnaeus, 1758

Korongo hawa ni ndege wa familia ya Ciconiidae wenye domo refu na nene (korongo wa familia ya Gruidae wana domo fupi na jembamba zaidi). Wanaitwa kongoti pia, hususa korongo mfuko-shingo. Mabawa yao ni marefu sana, yale ya korongo mfuko-shingo yana 3.2 m: marefu kuliko yale ya ndege wote ghairi ya tumbusi wa Andes (Andean condor).

Spishi nyingine huishi mahali pa majimaji nyingine mahali pakavu. Hula vyura, samaki, wadudu na nyungunyungu, hata ndege na wanyama wadogo. Korongo hawa hawawezi kutoa sauti. Lakini kwa tago hupiga kelele na domo yao.

Spishi wa Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi wa mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]