Nenda kwa yaliyomo

Domomundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Domomundu
Domomundu domo-jeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Phoeniculidae (Ndege walio na mnasaba na goregore)
Jenasi: Rhinopomastus
Jardine, 1828
Ngazi za chini

Spishi 3:

Domomundu, kwembemundu au hanjari ni ndege wa jenasi Rhinopomastus katika familia Phoeniculidae. Wanafanana na goregore lakini domo lao limepindika zaidi. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mng'ao buluu wa metali. Hula wadudu ambao wanawatafuta katika nyufa ya miti kama vigong'ota. Jike huyataga mayai 2-4 ndani ya tundu ya mti na kuyaatamia. Wakati huu dume amletea chakula.