Kiongozi (ndege)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiongozi
Kiongozi mabaka
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Indicatoridae (Ndege walio na mnasaba na viongozi)
Jenasi: Indicator G.R. Gray, 1855

Melichneutes Bonaparte, 1850
Melignomon Hermann, 1783
Prodotiscus J. Verreaux & E. Verreaux, 1855

Viongozi, vijumbe, walembe au ndege wa asali ni ndege wadogo wa familia Indicatoridae. Kwa kawaida jina “mlembe” hutumika kwa spishi za jenasi Prodotiscus na “kiongozi” kwa spishi nyingine. Ndege hawa wana rangi za kijivu, kahawa na nyeupe, pengine njano pia. Wabobea kwenye kula nta, kwa kawaida nta ya nyuki, lakini walembe na spishi ndogo za viongozi hula nta ya wadudu-gamba. Wanaitwa kiongozi kwa sababu spishi kadhaa (kiongozi mkubwa hasa) huongoza watu na wanyama kama nyegere mpaka masega ya nyuki. Watu au nyegere wakimaliza kutoa asali, kiongozi ala nta inayobaki. Viongozi hula majana, mafunza ya nta, wadudu wengine na buibui pia, na hata matunda mara kwa mara.

Viongozi hawatengenezi tago lao lenyewe. Jike hulitaga yai moja katika kila moja la matundu 5 au 6 ya spishi nyingine ya ndege, mara nyingi zile za vigong'ota, zuwakulu na goregore lakini walembe huchagua matago ya mviringo ya vinengenenge, videnenda, magamaga na vibwirosagi. Jike mmoja anaweza kuyataga mayai 20 katika mwaka mmoja. Domo la kinda la kiongozi lina kikulabu kinachotumika kwa kuyatoboa mayai ya mwenyeji na kuwaua makinda yake.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]