Nenda kwa yaliyomo

Kiseleagofu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiseleagofu
Kiseleagofu koo-jekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Picidae (Ndege walio na mnasaba na vigong'ota)
Nusufamilia: Jynginae (Ndege walio na mnasaba sana na viseleagofu)
Jenasi: Jynx
Linnaeus, 1758
Spishi: Angalia katiba

Viseleagofu ni ndege wa jenasi Jynx, jenasi pekee ya nusufamilia Jynginae katika familia Picidae. Wanafanana na vigong'ota wadogo lakini domo lao ni dugi na fupi zaidi. Kwa hivyo hutafuta wadudu na mabuu katika miti na matawi yanayooza au ardhini; hula chungu, samesame na siafu hasa.

Ndege hawa wana rangi ya kamafleji: nyeupe, kijivu na kahawia; manyoya yao yamechorwa kwa milia myembamba mingi iliyo myeusi. Wakitishwa wanaweza kulinyoosha koo lao na kukigeuza kichwa chao takriban nyuzi 180 kwa kila upande, wakati huo huo hufanya sauti ya sss kama nyoka. Jike huyataga mayai 7-9 katika tundu la kigong'ota.