Kamafleji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samaki ya wayo anaonyesha kamofleji ya kufanana na mchanga kwenye sakafu ya bahari

Kamafleji (kutoka kwa Kiingereza camouflage) au majificho ni hali ya kujificha kwa kujifananisha na mazingira.

Kamafleji inatumiwa na wanyama wengi kama kinga dhidi ya maadui lakini pia na wanyama wanaowinda wengine kama usaidizi wa kukaribia windo lao.

Inatumiwa pia na wanadamu, hasa na wanajeshi na wawindaji kwa njia ya kuchagua nguo zenye rangi na ruwaza zisizotambuliwa kirahisi.

Kamafleji kwa njia ya rangi[hariri | hariri chanzo]

Wanyama wengi huonyesha rangi inayolingana na makazi yao ya kawaida. Charles Darwin alitambua ya kwamba inasaidia katika mchakato wa uteuzi asilia kama rangi fulani inapunguza hatari ya kiumbehai kutambuliwa na kuliwa na maadui.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamafleji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.