Vumatiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Vumatiti
Vumatiti mdogo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama makorongo)
Familia: Ardeidae (Ndege walio na mnasaba na koikoi)
Jenasi: Botaurus Stephens, 1819

Ixobrychus Billberg, 1828
Tigriornis Sharpe, 1895
Tigrisoma Swainson, 1827
Zonerodius Salvadori, 1882

Spishi: Angalia katiba

Vumatiti ni ndege wakubwa wa nusufamilia Botaurinae na Tigrisomatinae katika familia ya Ardeidae ambao wana domo refu na nyembamba lakini shingo fupi kuliko spishi nyingine za familia hii. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, nyeusi na kahawia. Vumatiti hula samaki, amfibia na wadudu wa maji. Hizi ni spishi zinazojificha ndani ya uoto. Hujenga tago lao kwa matawi, manyasi na mimea ingine katikati ya matete au juu ya miti. Tago limefichika kwa kawaida.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]