Hua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hua
Hua kijivucheusi (Streptopelia lugens)
Hua kijivucheusi (Streptopelia lugens)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Columbiformes (Ndege kama njiwa)
Familia: Columbidae (Ndege walio na mnasaba na njiwa)
Nusufamilia: Columbinae (Ndege walio mnasaba na njiwa)
Ngazi za chini

Jenasi 6:

Hua ni ndege wa jenasi mbalimbali wa nusufamilia Columbinae katika familia Columbidae. Spishi nyingine huitwa tetere, kuyu au fumvu. Wana rangi kijivu, kahawia na nyupe na spishi nyingi zina rangi pinki. Jenasi ya Streptopelia inatoka Afrika lakini spishi kadhaa zimeingia Ulaya na Asia. Hua mkufu wa Ulaya na hua madoa (Spotted Dove) wamewasilishwa katika Marekani. Hua hula mbegu, matunda, mimea na pengine wadudu. Hulijenga tago lao la vijiti kwa miti au miwamba au ardhini kati ya manyasi. Jike huyataga mayai mawili kwa kawaida.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]