Majadiliano:Hua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

"Dove" kama taashira ya dini[hariri chanzo]

Je, makala hii inahusu Columbidae kwa jumla au Streptopelia hasa? Ningependa kuongeza sentensi kadhaa juu ya hua katika historia ya dini (Ukristo) na sanaa (Hua kama alama ya amani - mfano Picasso...). Madhani ingekuwa hapa lakini nasita kwa sababu sina uhakika vipi Columba? --Kipala (majadiliano) 14:49, 31 Agosti 2008 (UTC)

Ukitaka kuandika kuhusu "dove" kama taashira ya dini, lazima ujue kwanza "dove" wa dini Ukristo ni spishi gani? Kwa lugha za kirumi taashira hii inaitwa "columba" au "colomba", lakini majina haya hayamaanishi spishi au hata jenasi moja. K.m., kwa Kiitalia spishi nyingi za jenasi Columba huitwa "piccione", ingawa nyingine huitwa "colombaccio". "Dove" wako akiwa spishi ya Columba, basi tumia "njiwa". Vinginevyo tumia "hua". Majina mengine, kama "tetere" na "pugi", hayajulikani sana. ChriKo (majadiliano) 17:26, 15 Desemba 2014 (UTC)
Nadhani spishi kamili ya hua katika Biblia na penginepo haitajwi (katika kamusi kwa Agano la Kale naona columbia livia na columbia turtur - Agano Jipya haohao? Na Columbia Turtur - je hadi leo anaitwa vile?). Lakini swali langu ni kama makala hii inahusu Streptopelia hasa au kama tunaweza kuitumia kwa Columbidae kwa jumla? Kama ni vile naweza kuongeza habari za kiutamaduni kuhusu hua hapa (si kwa makala za spishi). Kipala (majadiliano) 21:11, 15 Desemba 2014 (UTC)
Sifahamu sana kwa sababu unataka kuweka habari ya kiutamaduni kuhusu hua/njiwa katika makala kuhusu Columbidae wote. Kwa Kiingereza watu wamechagua “dove” kwa taashira hii, kwa sababu hakuna tofauti hasa baina ya “dove” na “pigeon”. Kwa hivyo nafikiri haidhuru jina gani unachagua kwa Kiswahili. Ukipendelea hua ni sawa tu na kwa wazo langu ungeweka matini yako katika makala ya hua kama ilivyo. Sioni haja kuibadilisha ili ihusu Columbidae wote. Njiwa na pugi ni tofauti na hua, lakini labda ni mwanabiolojia anayeongea. Labda ungeuliza msemaji wa kienyeji.
Hivi, Columba turtur huitwa Streptopelia turtur siku hizi. ChriKo (majadiliano) 21:21, 17 Desemba 2014 (UTC)