Fimbi
Jump to navigation
Jump to search
Fimbi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 4 na spishi ?? za fimbi:
|
Fimbi ni jina linalotumika kwa spishi ndogo za familia ya ndege Bucerotidae; spishi moja inaitwa kwembe au kwembekwembe pia. Spishi kubwa za familia hii zinaitwa hondohondo. Fimbi wana domo kubwa lakini lile halina aina ya pembe juu lake kama domo la hondohondo au pembe hii ni dogo sana. Domo linaweza kuwa jeusi, jekundu au njano. Isipokuwa fimbi wadogo, spishi za Afrika zinatokea savana kavu na spishi za Asia zinatokea misitu. Fimbi hula matunda, mbegu, wadudu, mijusi na panya.
Jike wa fimbi huyataga mayai 2-6 katika tundu ya mti au mwamba, pengine katika tundu ya kigong'ota au zuwakulu. Dume afunga mwingilio wa tundu kwa matope, mavi na nyama ya matunda. Awaletea jike na makinda chakula.
Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]
- Horizocerus albocristatus, Fimbi Ushungi-mweupe (White-crested hornbill)
- Horizocerus hartlaubi, Fimbi Mdogo Mweusi (Black Dwarf Hornbill)
- Lophocerus alboterminatus, Kwembekwembe (Crowned Hornbill)
- Lophocerus bradfieldi, Fimbi wa Bradfield (Bradfield's Hornbill)
- Lophocerus camurus, Fimbi Mdogo Domo-jekundu (Red-billed Dwarf Hornbill)
- Lophocerus fasciatus, Fimbi Rangi-mbili (African Pied Hornbill)
- Lophocerus hemprichii, Fimbi wa Hemprich (Hemprich's Hornbill)
- Lophocerus nasutus, Fimbi Mweusi (African Grey Hornbill)
- Lophocerus pallidirostris, Fimbi Domo-jeupe (Pale-billed Hornbill)
- Tockus damarensis, Fimbi wa Damara (Damara Red-billed Hornbill)
- Tockus deckeni, Fimbi wa Decken (Von der Decken's Hornbill)
- Tockus erythrorhynchus, Fimbi Domo-jekundu Kaskazi (Northern Red-billed Hornbill)
- Tockus flavirostris, Fimbi Domo-njano Mashariki (Eastern Yellow-billed Hornbill)
- Tockus jacksoni, Fimbi wa Jackson (Jackson's Hornbill)
- Tockus kempi, Fimbi Domo-jekundu Magharibi (Western Red-billed Hornbill)
- Tockus leucomelas, Fimbi Domo-njano Kusi (Southern Yellow-billed Hornbill)
- Tockus monteiri, Fimbi wa Monteiro (Monteiro's Hornbill)
- Tockus ruahae, Fimbi wa Tanzania (Tanzanian Red-billed Hornbill)
- Tockus rufirostris, Fimbi Domo-jekundu Kusi (Southern Red-billed Hornbill)
Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]
- Ocyceros birostris (Indian Grey Hornbill)
- Ocyceros gingalensis (Ceylon Grey Hornbill)
- Ocyceros griseus (Malabar Grey Hornbill)