Keremkerem

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Keremkerem
Kerem kidari-marungi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Coraciiformes (Ndege kama viogajivu)
Familia: Meropidae (Ndege walio na mnasaba na keremkerem)
Jenasi: Meropogon Bonaparte, 1850

Merops Linnaeus, 1758
Nyctyornis Jardine & Selby, 1830

Spishi: Angalia katiba

Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana rangi maridadi na mwili wao ni mwembamba. Domo lao ni refu na jembamba na mkia wa aina nyingi ya keremkerem una mileli mirefu katikati.

Ndege hawa wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, na nyuki, manyigu na mabunzi hasa, ambao wanakamatwa hewani. Kabla ya kula, ndege anatoa mshale wa mdudu akimgongia tawi la mti au kitu kigumu kingine.

Keremkerem hupenda kuwa pamoja kwa makundi. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga kwa kutaga mayai yao meupe.

Familia ya Meropidae imegawika nusufamilia mbili: Nyctyornithinae (keremkerem wenye ndevu) na Meropinae (keremkerem wa kawaida).

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]