Mto Koreni
Mto Koreni ni kati ya mito ya mkoa wa Tanga (Tanzania Mashariki) ambayo maji yake yanaishia katika Bahari Hindi.
Mto Koreni una misitu minene ambayo imebahatika kuwa na chemchemi kadhaa zilizoenea kila sehemu pembezoni ya misitu hiyo. Kwa upande wa Pangani na Muheza misitu hiyo upande wa magharibi mwa shamba la mkonge maarufu kama Amboni Estate au wengine huita Bago Estate.
Wakazi wa maeneo ya jirani kama kijiji cha Kimang'a, Boza Bago na mengineyo kipindi hicho kimang'a hakuna mabomba ya Maji.
Pia misitu hiyo inatumika kufanya matambiko kwa mizimu mbalimbali ili kuondoa mikosi na kufanikisha mambo; mara nyingi imehesabiwa kutisha na kuwa na maajabu mengi. Wengine huamini maji ya mto huo kuwa na baraka nyingi kwani wengi husafiri kutoka mbali kuufuata mto huo ili kupata baraka zake.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Koreni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |